MLANGO WA IMANI UMEFUNGULIWA KWA AJILI YAKO


open-doors MLANGO WA IMANI UMEFUNGULIWA KWA AJILI YAKO

Mlango mkubwa wa kufaa sana umefunguliwa , Lakini kuna wanaokupinga ni wengi  sana.  Yesu anasema , Basi enendeni  mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi .Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha, jitieni nira yangu , mjifunze kwangu. kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.  nanyi mtapata raha nafsini mwenu ; kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.

Anasema tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia.  Tunaendelea na matangazo ya kazi za imani. Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki  yake na hayo yote unayosumbukia leo utazidishiwa.

Mtu yeyote anayesema hakuna kazi , mtu kama huyu inajulikana kwamba Hana UPENDO. Kwa sababu kazi ziko nyingi  sana .  Ukikosa Upendo huwezi kuona kazi ,wewe kama  huoni kazi  ina maana huna upendo na  kuna vitu vinakuzuia usione kazi.  mahali penye kazi ndiko ambapo utakutana na Mungu.  Kama una kazi kupata kazi ni rahisi, lakini kama huna kazi kupata kazi ni ngumu . Mwenye kitu huongezewa  lakini asiye na kitu hata kile kidogo alicho nacho hunyang’any’wa.

1.Ukienda kufanya usafi wa mazingira  kwa kutambua kuwa unaenda kazini, utakutana na Mungu  huko huko atakupangia kazi unayotaka.

2.Ukienda kuwasaidia watoto Yatima utakutana na Mungu atakupangia kazi

3. Ukienda kwa Wagonjwa  utakutana na Mungu huko huko atakupangia kazi.

4 Ukienda kwa wafungwa kuwapa faraja au hata kuwapelekea sabuni  utakutana na Mungu huko  atakupangia kazi

5.Ukienda kuwasaidia wajane  utamkuta Mungu  huko na atakupangia kazi yako ya kudumu.

Mungu anataka aone kuna kitu unafanya cha kwake kwanza ndio akupe cha kwako unachokitaka.

Ukitoa MUDA Kwa ajili ya hizo kazi za imani , lazima muda wako uongee.  Muda unakuletea kila kitu,  Muda utakupa mafanikio na muda huo huo utakuletea umasikini usipotumia vizuri.

MLANGO WAKO WA IMANI UMEFUNGULIWA LAKINI WANAOKUPINGA NI WENGI.

Maadui hawa ni kina nani,

Aibu

Mashaka

Hofu

Wasiwasi

Smartphone.  kama huna nidhamu nayo

Watu

T.v

Ujinga ,Maradhi, Umasikini, Magonjwa

Wanakuzuia usifike unakotaka kwenda. ng’ombe anamjua bwana wake, na punda anakijua kibanda  cha bwana wake, lakini watu wa Mungu  HAWAFIKIRI . Nchi yenu ni ukiwa, miji yenu imeteketea, wageni wameila mbele ya macho yenu, mlangho wako wa imani  ni nani amefunga? Ni mlango upi ambao Mungu atakukuta ili akupangie kazi?

Ka,ma wewe ni mfanyakazi , umeajiriwa, je ni mwaminifu?  unawahi kazini?  huchukui Rushwa?  Unatumiaje Muda wako. Kumbuka Mungu hana upendeleo,  Ukiwa mwaminifu kazini lazima  Mungu atakupa kazi nzuri unayoitaka. Kama utakuwa unapenda vitu hivi vitatu.

Mpende Mungu

Penda Mazingira 

Penda Watu.

Kazi za imani ni za kudumu , lakini kazi za kuona ni za muda mfupi tu.

Ukipata kazi kwa kutoa rushwa , hio kazi sio ya imani, ni ya laana, haitadumu. Lakini kazi za imani  ni kufanya kazi ya Mungu kwanza ili Mungu akupangie kazi , hio ni ya kudumu.

Kwa hio pambana na maadui ambao wanakuzuia  kuona mlango wako mkubwa uliofunguliwa , mlango wa imani. Acha kupambana na shetani, pambana na woga, hofu, wasiwasi, ujinga, mashaka,  na maadui wengine wanaokujia wewe.  Maana Mungu hakutupa roho ya woga bali  ya nguvu  na ya upendo na ya kiasi.

Shinda aibu kama Yesu alivyoshinda aibu yake , alipambana na Aibu  sio shetani. alipambana na hofu sio shetani. Sasa ndugu unapigana na shetani   mpaka lini , wakati hata hana shida na wewe. Wewe ndio shida.

Kubali kulipa gharama kwanza , usipende kupokea tu, matokeo yake sio mazuri.

Subscribe  ili kupata mafunzo mapya kila mara.

 

Previous FIKIRI MABADILIKO  (THINK FOR CHANGE)
Next UKITAKA MPENYO FIKIRI KAMA MTUMISHI

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.