Mume Akataka Talaka, Kwa nini?, Kwa Sababu Eti Mke Hafanyi Kazi:


hqdefault-1 Mume Akataka Talaka, Kwa nini?, Kwa Sababu Eti Mke Hafanyi Kazi:

AKAENDA KWA MSHAURI KUULIZA;,

Hili ni somo zuri kwetu sote, haijalishi  upo hatua gani katika maisha yako ya ndoa. utaoona namaanisha nini hapa.

Mwanaume alichanganyikiwa kwa ajili ya mke wake kwa kutofanya kazi.na kutowajibika ipasavyo katika maswala ya ndoa , ndio maana akaenda kwa mshauri ili ajue jinsi ya kupata talaka , na haya ndio yalikuwa mazungumzo yao.

MSHAURI: Unafanya kazi gani Mr.?

MUME: Ni mhasibu wa Benki

MSHAURI: Mkeo je?

MUME: Hafanyi kazi ni mama wa nyumbani.

MSHAURI: Nani anatengeneza breakfast ya  familia nzima?

MUME: Mke wangu kwa sababu yeye hafanyi kazi.

MSHAURI:Muda gani mke wako huamka asubuhi?

MUME: Huamka mapema sana kabla ya mtu yeyote, kwa sababu inabidi ajipange  kwa ajili ya kutengeza chakula cha watoto cha mchana  huko shuleni. ahakikishe wameoga vizuri, wamepiga mswaki vizuri, wamevaa vizuri, na wamechana nywele zao vizuri, na wapate chai kabla ya kuondoka.pia ahakikishe watoto wamechukua kila kinachohitajika shuleni.

Na wakati huohuo  mtoto mdogo huamka,  humbadilisha nepi na kumnyonyesha  na kumbadilishia nguo. na pia kutengeneza kitafunio kwa wote.

MSHAURI:Watoto wako wanaendaje shule?

MUME: Ni mke wangu huwapeleka shule kwa sababu hafanyi kazi.

MSHAURI: Baada ya kuwapeleka hufanya nini tena?

MUME: Kwa kawaida hufanya vile ambavyo hakukamilisha kuvifanya wakati alipokuwa huko shule, huenda kulipa bili mbalimbali na kwenda sokoni kwa ajili ya kununua mahitaji, na wakati mwingine husahau vitu na kurudi tena huko sokoni na akiwa na mtoto mgongoni mwake.

Akirudi nyumbani huanza kumlisha  tena mtoto na kumbadilisha nepi , kusafisha jikoni na kufua na kusafisha nyumba nzima , kama ujuavyo, si   kwa sababu hafanyi kaziii.

Hyatt-Place-St-Louis-Chesterfield-P014-Kitchen-Skillet-Buffet-1280x427-1024x342 Mume Akataka Talaka, Kwa nini?, Kwa Sababu Eti Mke Hafanyi Kazi:

MSHAURI:Jioni ukiridi kutoka ofisini unafanya kitu gani?

MUME: Napumzika. nakuwa nimechoka siku nzima nimefanya kazi.

MSHAURI: Mke wako usiku anafanya nini?

MUME: Anatengeneza chakula cha usiku, ananiandalia mimi na watoto, anaosha vyombo, anaweka nyumba vizuri tena, anahakikisha mbwa wamekula na kuwafungulia, baada ya kuwasaidia watoto homework, anawaandaa kwa ajili ya kulala , anawabadili nguo na kuwavalisha za kulalia, anambadilisha mtoto nepi yake na  kumpa maziwa ya uvuguvugu.

Baada ya hapo hukagua vitu vyote na kuja kitandani kulala,ananza kumnyonyesha mtoto tena na kumbadilisha nepi usiku  tukiwa tumelala inapobidi.kwa sababu hataki  mtoto aamuke.

MSHAURI: Bado unahitaji  talaka sasa?

MUME: Hapana. hapana, nataka kurudi nyumbani kwangu sasa na kumpa mke wangu pole na kumshukuru.

Hizi ndizo kazi za kila siku za wanawake wote duniani, anaaanza asubuhi na kuendelea mpaka saa za usiku, na  hii inaitwa HAFANYI KAZI?!

Kuwa mama wa nyumbani  huna Diploma, lakini  umeshikilia ufunguo wa usalama wa maisha ya familia nzima na kutawala.

Furahia na mkubali mke wako, mama , bibi, binti, kwa sababu wanajitolea  bila malipo.

Mtu mmoja akamuuliza huyo mama, .wewe ni mwanamke  mwenye kazi au mama tu wa nyumbani”??

Mama akajibu..

Nafanya kazi kama mke nyumbani masaa 24 kwa siku , kila siku.

Mimi ni mama.

Mimi ni  mwanamke.

Mimi ni binti.

Mimi ni kengele ya kuwaamsha kila mtu nyumbani.

Ni mpishi.

Mimi ni mfanyakazi wa ndani.

Mimi ni bwana .

Mimi ni mhudumu.

Mimi ni yaya.

Mimi ni nurse.

Mimi ni kama mbeba zege.

Mimi ni mlinzi wa nyumba.

Mimi ni mleta amani.

Mimi ni mshauri.

Sina mda wa kutoka kwenda kwa marafiki.

Sina kibali cha magonjwa.

Sina siku ya mapumziko.

Nafanya kazi usiku na mchana.

Niko zamu muda wote.

Sipokei mshahara.

Hata hivyo  ni mara chache nasifiwa, wewe unafanya nini kwa siku nzima?

Huu ni  mwaliko kwa wanawake wote wanaohudumia familia  na kushikilia maisha  yao yote. mwanamke ni kama CHUMVI.

Uwepo wake haukumbukwi, lakini asipokuwepo kila kitu kinakosa ladha.

soma hii pia.,

NANI HUBEBA MZIGO MZITO?, JE NI MUME AU MKE?

 

shirikisha familia  na marafiki makala hii.

 

 

 

Previous JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:
Next JE, SEX INAKUSAIDIA KUPATA MAPENZI YA KWELI??..!

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.