MWONGOZO WA KWELI KATIKA NIA ZETU ZA NDANI


30979-manprayingintext MWONGOZO WA KWELI KATIKA   NIA ZETU ZA NDANI

Ulimwenguni kuna dini mbali mbali, Dini hizi haziaminiani zenyewe kwa zenyewe , kwa sababu kila dini ina imani yake na njia yake . Lakini zote hizo ni kwa ajili ya lengo la kumfikia Mungu.Hakuna njia moja.

Haijalishi ni njia gani unapitia , ilimradi unatembea katika haki  ndani ya vitu viwili muhimu sana, navyo ni ,

1.Maono ya malengo

2.Kuamini  kwamba unacho chanzo cha kukufikisha kule unakoelekea.

jews MWONGOZO WA KWELI KATIKA   NIA ZETU ZA NDANI

Uwezekano wa kukufikisha kule ni kuwa na shauku ya  kutafuta  ukweli kuhusu vitisho, woga na wasiwasi, kujitahidi kuwa mtakatifu,  kushughulika na matarajio yako, kujaribu, na kufurahia. ndio uchaguzi mzuri utakaofanya katika  safari yetu hii.

Ufahamu ni zaidi ya  mawazo, na ni zaidi sana kuliko hata kazi ya  ubongo wako, ufahamu ni zaidi ya shamba kubwa, sio tu kwa kuwa hauonekani bali  hauhitaji nguvu.

Shamba hili la ufahamu ni  nyumba yetu ya kweli , na ufahamu huo umekusanya  mageuzi makubwa na sio ya kimwili wala ya kiroho tu ni zaidi ya haya. Nyumba yao yote ni mwanga ambao sio mali yako , mwanga huo huja kwa  wanaohitaji.

Mfano. Unaweza ukawa unatembea mahali , halafu ukahisi kama kuna mtu anakufuatilia nyuma yako , na ukitaka kuhakikisha unakuta ni kweli kuna mtu anakufuatilia nyuma, au wakati mwingine  unaweza ukawa unasikiliza hotuba nzuri  na ukawa unajua kitu gani kinafuatia  baada ya hapo , na mnaweza kumalizia neno kwa pamoja .

Mwili mmoja na akili moja  lakini unaishi nje ya shamba la ufahamu mwenyewe.

Utawezaje kuwasiliana na Mungu?

Kama taa ilivyofunikwa ndani ya ndoo, ndivyo roho yako ilivyofunikwa  na mwili kwa maana kwamba hakuna anaekujua wewe , ni wewe na roho yako ndani, usiwe gizani, tamani mwanga. usiruhusu hili liwepo  kwako ili ufahamu wa roho ujionyeshe wazi  ndani yako na nje yako. kwa maneno mengine ni kwamba Ishi kulingana na  hatua ya roho yako kama unategemea wengine waamini kwamba   Unamwamini mungu.

Kujaribu kujifungia ndani ya box na kuweka lable yenye sifa ya kwamba unampenda mungu kumbe hio ni lable tu  sio nzuri . Ni kosa  la kujaribu  kumweka mungu ndani ya hilo box. hakuna kinachofanyika  kizuri kwako .

Mpende bwana mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. 

Hii nitakuja kuielezea siku nyingine jinsi gani ya kumpenda mungu kwa moyo, roho ,akili, na nguvu.

Lakini  nakuahidi kukuletea mwendelezo wa somo la leo  Jumapili ijayo  tufahamu  mwongozo  ulihakikishwa na wachunguzi  wengi  kuwa zina nguvu katika  kumtafuta mungu. tutaangalia jinsi ya kufahamu nia na mengine yanayofanana na hayo.

PrayingHands MWONGOZO WA KWELI KATIKA   NIA ZETU ZA NDANI

Uwe na siku njema, Barikiwa.

 

 

 

Previous NGUVU YA NIA KATIKA KUMTAFUTA MUNGU.
Next SABABU KUBWA ILIOJIFICHA KWA NINI NDOA ZINAVUNJIKA

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.