Natumaini Mwaka 2017 Ni Mwaka Ambao Umekufundisha Maumivu Makali Ya kutosha


DCoIhFlVwAAa8uA Natumaini Mwaka 2017 Ni Mwaka  Ambao Umekufundisha Maumivu Makali Ya kutosha

Umejifunza kitu fulani ambacho ni kigumu kiasi kwamba  ulijaribu kumbadilisha mtu lakini hukuweza.

Umenijifunza, hata mimi nimejifunza kuwa watu tunaowataka sio ambao tunawapata.

Tumejifunza kwamba badala ya kujaribu  kutumia nguvu nyingi na ngumu sana ,  umeona kumbe ni bora kujiponya kuliko kuendelea kuteseka.

Tumejifunza kuachana na yaliopita, hakuna kung’ang’ana na yaliopita.

Tumejifunza kwamba, kusubiri watu wakuthibitishe kwenye instagram, facebook kwa kukupa tiki zao ili uonekane kuwa ni mzuri au unafaa , sio dili hata kidogo, badala yake ni  kutambua kuwa kitu cha hovyo hakina maana. ni bora kujithibitisha mwenyewe.

Tumejifunza kwamba , haijalishi mtu atasema nini juu yetu , sio biashara yetu, Tumetambua kuwa kusemwa hakuishi hata kama uwe wa aina gani utasemwa tu. uwe mnene utasemwa, uwe mwembamba utasemwa. uwe tajiri utasemwa, uwe maskini utasemwa.  huwezi kuzuia kusemwa.

Tumejifunza kujiamini wenyewe japo kidogo.   Dalili mbaya zinapokuja ni rahisi kuziepuka .

Tumejifunza kutomwamini  mtu mapema na kumwambia kila kitu . kwa  sababu sio kila mtu anastahili.

Kujifunza kuuliza maswali ili kufahamu, na kama utaona hawezi kujibu ni bora kubadilisha maswali ili mtu ajisikie huru kujibu.

Tumejifunza kudharau meseji ambazo hazina maana katika maisha yetu ili zisiharibu uzuri wa furaha tuliyonayo katika maisha yetu.

Mimi nimejifunza kwamba , Hata kama nataka kuongea na mtu sitakiwi kuanzisha mazungumzo.

Nimejifunza kwamba kama mtu anataka kuwa na wewe atakuja tu.

Jifunze kuwa kuna watu ambao wanachanganya  signals, unajaribu kuzielewa lakini huwezi, kwa sababu sio za kwako.

Jifunze kwamba  kuna marafiki vigeugeu ambao hawawezi kuchukua muda mrefu kuwafahamu kuwa ni wanafiki kwako. usiudanganye moyo wako, jiamini wewe mwenyewe.

Jifunze kutokutoa siri zako kwa marafiki. hakuna rafiki mwema kwako. akiwepo ni mmoja kwa mia.

Jifunze kuwa kuna marafiki wanaotaka faida kwako. lakini hawakuheshimu hata kidogo.

Jifunze kuondoka kwenye mahusiano ambayo  hutaki kuwa nayo maishani mwako, mahusiano yenye kuleta maumivu kwako. Ni watu ambao hawatakuelewa.

Jifunze kwamba sio kazi yako  kuboresha ujasiri  wa moyo wa mtu.

Jifunze kuwa sio kwa sababu una historia nzuri  kwamba utakuwa na maisha mazuri, haina maana kuwa utapata maisha mazuri baadae.

Jifunze kuwa hutakiwi kuishi na maumivu uliyonayo, lakini tambua kuwa  sio sehemu ya maisha yako pia.

Jifunze kwamba , kama unataka kupendwa na kuheshimiwa na watu , lazima kwanza  uanze kuwaheshimu na kuwapenda watu kwanza.  ukitaka kufanyiwa vizuri , wafanyie watu wengine vizuri kwanza.

Panda mbegu nzuri , Utavuna matunda mazuri.

Uwe na mwaka mpya mwema.

Subscribe.

Previous Njia 7 Za Kutumia Muda Peke Yako Zitabadilisha Maisha Yako
Next Mambo 10 Mazuri Ambayo Yatatokea Mara Tu Utakapoacha Kuwaza Kuhusu Watu Watanionaje

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.