Ndoa Inayobebeka Ni Ipi Nyakati Hizi


1154006

Chombo chochote kisichokuwa na vishikio  hakiwezi kubebeka. Mfano beseni lisilo na mashikio yake hutaweza kulibeba.

eliza-1 Ndoa Inayobebeka Ni Ipi Nyakati Hizi
12

Ndoa nyingi zimepoteza changamko ,Hazina ladha . Changamko ni dawa ya ndoa Au ni kama mate yaliopo ndani ya mdomo wa mtu ambayo husaidia mtu kuongea kwa sababu ya utelezi  uliopo ndani.

Watu wengi wanaingia kwenye ndoa bila ya kujua taarifa sahihi za ndoa. Wengi wanafikiri ni kawaida , wengine wanasema ni kuondoa nuksi,  mwingine kwa kuwa anaona watu wanaoa na kuolewa, Mwingine kwa kuwa anataka kila akihitaji tendo la ndoa kuna mtu amabaye atastarehe naye bila ya kuhangaika huko nje.

Hawatafuti maana halisi ya ndoa. wanafikiri ni kuolewa na kuzaa halafu kufa basi. Hilo sio kusudi la ndoa.  Kama hutaweza kutumia muda wako ili kutafuta taarifa sahihi, kutafuta maarifa na kufahamu kuhusu ndoa, hutaweza kudumu kwenye ndoa, hata kama utadumu lakini ni kwa mateso makubwa sana. kuvumilia. hutafurahia ndoa.

Kanuni Zinazoleta Vibebeo Vya Ndoa.

1.Mvuto

Ndoa nzuri ni ile ambayo mtu anatambua madhaifu yake na kuanza kubadilika mwenyewe badala ya kutaka kumbadilisha mwenza wake.  Usipofahamu kuwa wewe ndio chanzo cha mabadiliko, Utaanza kutaka kumbadilisha mtu mwingine, kitu ambacho ni kigumu na hakiwezekani. Ukifanya hivyo ni sawa na kusukuma upepo.

Ukiweza kujibadilisha baadha ya maeneo ya madhaifu yako , hapo utasababisha mwenza wako kufuata sheria zako  au tabia zako nzuri . Achana na matendo ya kale , yaani tabia za nyumbani kwenu ulikotoka  kwa sababu upo kwenye Agano lingine . Nalo ni Agano la ndoa.

2.Mawasiliano

Mawasiliano ni kitu cha kwanza kabisa kati ya watu wawili . Ni lazima kiwango cha mawasiliano kiwe cha juu.  Penye taarifa sahihi pana mafanikio makubwa. Palipo na usemi mmoja, nia moja, kusudi moja. Hivi vitu vitoke ndani ya mtima wa moyo wa mtu hapataweza kuharibika kitu.

Ngazi 4 Za Mawasiliano

1.Matukio

Kuna wanandoa wakikaa pamoja ni kuongea kuhusu matukio yanayotokea tu, hakuna kingine. Mfano mambo yaliofanyika siku hio kazini, barabarani, harusini. Haya ni mawasiliano duni sana.

Wanandoa wa aina hii wanaishi kwa kuvumiliana, ilimradi siku ziende, Lakini hawana furaha ya ndoa, mahusiano yao sio ya kweli, Huenda ni kwa sababu tu watunze watoto. Maana watoto imekuwa kamba ya kufungia Nira. Ndio maana wako pamoja

Wana migogoro mingi na wamekinaiana. Kila mtu amemkinai mwenzake. Makelele mengi. Mwili upo kwa mume au mke , lakini moyo upo kwingine.

2.Mambo Ya Familia

eliza-2-1024x683 Ndoa Inayobebeka Ni Ipi Nyakati Hizi
bills

Wanaongea kuhusu familia, Ada za watoto , afya za watoto,  mambo ya pesa, ndugu, maendeleo ya watoto shule. Hakuna mambo mengine.

3.Hisia Za Ndani.

Ni muhimu sana kuongea juu ya hisia za ndani.  Kuhusu maumivu anayopata mwenzi wako, nani anasababisha . Ni wewe au yanatoka wapi. Moyo wa mwenzi wako unalia juu ya nini. Kuhusu hisia zako mwenyewe. kufungua moyo ili mwenzako aweze kufahamu tatizo lako

Black-couple-fight-relationship-sad-angry-unhappy-e1471357042435_690x450_crop_80 Ndoa Inayobebeka Ni Ipi Nyakati Hizi

Moyo umejeruhiwa na nini. Kwa kiwango gani. Utafanyaje kuponya moyo huo.  Ni muhimu kujua kitu gani kinamfurahisha na kipi kinampa huzuni ya moyo wake.

Kuna wenye Hekima wawili nimewasikia wakisema kuwa , kwenye ndoa mara nyingi Mume akitaka kufika kileleni , huvuta hisia kutoka mbali , anakumbuka mwanamke mwingine ambaye alifanya tendo  hilo na alimfurahisha , ndipo anaweza kufika kileleni. Unaipata hio . Kwa hio wengi wa wanawake hufikiri wamewafurahisha waume zao kumbe hakuwepo naye bali na mtu mwingine.

Lakini  sentensi hii iliniumiza sana mimi , nilitambua ni kwa kiasi gani hawa watu hawaongelei hisia zao wakiwa pamoja. Ni tatizo kubwa.

4.Majukumu.

Kila mwenzi ni lazima kutekeleza majukumu yake.  Mume abebe majukumu yake na mke pia abebe majukumu yake. majukumu yasipotekelezwa yanasababisha migogoro na mawasiliano kuwa mabaya.

Mungu anamtazama mwanaume kwa ukumbwa , lakini mwanaume hajitambui kuwa yeye ni kiongozi.

Mume ni Kiongozi wa familia , lazima afanye majukumu kama kiongozi. Ni kosa kubwa kumwachia mwanamke majukumu yake. Ni dhambi.  Mume ni kichwa  kwa sababu yeye amebeba misuli ya uongozi, mwongozo wa familia,  hasa kwa watoto wake, Amebeba hekima ambayo Mungu anatamani aingize kwa watoto, ana maarifa, maamuzi mazuri , Nidhamu. .Kumpenda mke, Mume ni mtoaji. lazima atunze mke, watoto.

Mke ni msaidizi na ni msimamizi, pia ni mlinzi wa mume wake. Kwa kusoma Neno la Mungu. Kubariki kazi za mume wake, kumpongeza, kumshauri.

Kuna wanawake hawajui kupika, hawafui nguo za waume zao, wala hawatekelezi majukumu  ya ndoa, hawatoi huduma nzuri ya ndoa. Wameachia msichana wa kazi kila kitu. Dada wa kazi ndiye anayefahamu boxer za baba zilipo, soksi za baba zilipo. mwanamke hajui, na wala haoni kama ni tatizo. huko ni kufunngwa Akili.

Tafuta maarifa ya kutosha kabla hujaingia kwenye ndoa. Usiingie kwa mkumbo. Usimsemi mume wako vibaya mbele ya marafiki zako, ndugu zako. Hatima ya mtu iko kinywani mwake.

Mume muombe Mungu kazi kwanza. Mke atakuja ili kusaport maono yako.

Mume mpende mke wako. Mke mtii mume wako na kumpa heshima.

Subscribe  kupata makala mpya kila inapokuja.

Previous Njia Rahisi Ya Kuondoa Tabia Mbaya Usizozipenda
Next Mwongozo Utakaokusaidia Kuondokana na Mawazo Mabaya

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.