NDOTO YANGU


husna2 NDOTO YANGU

Nilikuwa mtoto wa kawada  katika familia ,lakini nilikuwa ni  wale watoto wajanja  wajanja ,  nilipenda kufanya kazi ,hata mama yangu akawa ananiamini hata kama yupo safarini anakuwa hana mashaka  . Nilipenda kuwa mtangazaji ,nilipenda kusikia Betty mkwasa akitangaza  natamani nami siku moja niwe kama yeye,nilijitahidi kusoma kwa bidii na nikafaulu kwenda sekondari.

Nikiwa sekondari nilipata matatizo , niliumwa kwa muda mrefu bila kupana nafuu, nikashindikana hospitali ,nikarudi nyumbani , wazazi wangu wakashauriana kunipeleka kwa waganga wa kienyeji,huko nilitibiwa na kuambiwa ni nani mbaya , lakini katika akili yanu sikuwa na imani  hio.nilisumbuka sana lakini nilipona.

Niliendelea na masomo , nilipofika  kidato cha tatu , ndugu yangu ambae ndio kwanza alimaliza mafunzo ya  ualimu  na kupangiwa  kituo cha kazi, akafariki hata kabla hajamaliza  mwezi kazini. Iliniuma sana , na wakati huo ndio nilianza kujua kuwa kumbe kuna kifo.  Baada ya muda  wa kama miezi mitatu hivi akafariki dada yangu mwingine ,nilipenda sana na yeye alikuwa kama mfano  katika maisha yangu.

Iliniletea shida sana na kukata tamaa kabisa ya maisha, niliona hakuna faida ya kusoma , kwa sababu  dada huyu alipoenda jeshini    hata kabla ya kumaliza jeshi kafariki, ilikuwa ni vigumu kwangu kuamini kuwa nitaweza kumaliza shule.niliona nisafari yangu ilifuata baada ya hapo , maana kila mtu aliyetaka kufanikiwa alikufa , sasa mimi natafuta nini .nilimaliza shule kwa shida , sikuwa hata nasoma .

Nilipomaliza shule sikurudi nyumbani , nilienda kwa rafiki yangu ,huko niliona kama najiokoa na janga la kifo.  nilitafuta kazi , lakini niwaza je nikifa sasa nitakuwa sijapata hata mtoto, nikaamua kuolewa nikiwa na umri mdogo. kwa hio  nilianza maombi ya kuolewa  , kufunga kumwomba mungu  kwa bidii  ,hakuna mtu mkubwa ambae alielewa kama nipo kwenye msongo  wa  mawazo na woga wa kifo maana nilikimbia  kuogopa.

kwa hio sikutimiza ndoto yangu .Nataka ujifunze kitu hapa , kwamba ukiwa na tatizo usikimbie  bila kuhusisha wazazi wako na hata wakubwa zako ambao wapo watakusaidia , ili uweze kutimiza ndoto zako .kukimbia hakuleti jawabu ,badala yake utaongeza matatizo juu yake ,kwa kuwa kifokipo kila mahali  .