NGUVU ILIYOKO NDANI YA SONONEKO, SIKITIKO NA HUZUNI:


images-10 NGUVU ILIYOKO NDANI YA SONONEKO, SIKITIKO NA HUZUNI:

Sijui kama unaelewa kama dunia ya sasa imebadilika kiasi kwamba   huwezi hata kumsaidia mtu  au jirani  pindi panapotokea tatizo.  unaweza ukawa unapita sehemu ukaona mtu anapigwa lakini ukashindwa kumsaidia , ukabaki unaumia ndani ya moyo wako , kwa nini?   kwa sababu wanaweza kukugeukia wewe , ni bora ukatumia njia nyingine ya kuita msaada kuliko kujitosa wewe.

kwa hio inakubidi utumie ile njia ya kufikiri kwa haraka au taratibu ,  mimi naona hapa ni kuwa makini na maamuzi utakayochukua . sio kukurupuka . ulimwengu tunaoishi  sasa ni tofauti sana  , unaweza ukaona kuwa unafanya jambo zuri kumbe unajipeleka kwenye matatizo.

ikiwa wewe umejizoeza kufanya tafakari kila siku  itakusaidia katika maamuzi yako, kwa uzoefu wako mwenyewe ulimwenguni humu   tunaishi na kupita katika mambo magumu , bila ya msaada  wa akili iliotulivu utajikuta katika tatizo lisilo lako, lakini bado kuna nguvu ambayo huja kwa ajili ya wengine .

Unapoona kuna kitu kibaya kinatokea  , unatakiwa kutulia na kufanya maamuzi   yenye akili, na hio itakusaidia tu endapo una mazoea ya kutafakari. kwa sababu  , tafakari itakufungua akili na kuona mwanga wa   kuona endapo ni shida kubwa sana , na ni jinsi gani ya kutatua na kuweka sawa.

Wakati baraka inapoondolewa ,  na  ulikuwa bado unahitaji  kuona ukiendelea kuwa nayo,  unaanza kusema bora kama ungefanya vizuri isingeoondolewa.

Furaha inapotoweka, kunatokea shambulio kati yenu , hapo nako unaona ni jinsi gani  maumivu yanavyokuja.

Unapogundua umetenda kosa , na wakati huo uliemtendea hayupo.

Lionsgate-Children-Of-Sorrow_Bill-Oberst-Jr-Leach NGUVU ILIYOKO NDANI YA SONONEKO, SIKITIKO NA HUZUNI:

Unapotembelea wagonjwa hospitalini na kuona jinsi wanavyohangaika na maumivu, nawe utasikia kuumia moyoni.

Unapoenda kutazama wafungwa nako utasikia kuumia ndani yako.

unapotembelea wazee wasio na malezi  , utaona huruma pia.

Unapoona mwanamke amechoka na shughuli nyingi  , na kuona hali fulani sio ya kawaida usoni mwake,  na mwanamke huyo ni muuzaji wa  bidhaa za kutembeza,  lazima utasikia  kuumia ndani yako , na utaanza kusikitika , ndani ya mifupa yako  maumivu fulani .kama  huna msaada wowote kwake utaumia tu .

Kuna wakati mwingine   unapoona familia fulani iliotengana  na watoto kusambaratika,  pindi familia hio inapouungana tena  na kurejea pamoja , hapo nako utatokwa machozi ya  huruma  , na machozi ya sikitiko yakitiririka machoni mwako.

Unapoona kitu kibaya kinamtokea mtu umpendae,  nguvu hio inakuwepo kwako kama wewe  ndio uliyepatwa na hilo tatizo . unalisikia ndani yako   na kama amekosa amani nawe pia utakosa amani vilevile.

BILA YA HISIA HIZO BASI WEWE SIO MKAMILIFU

Unaweza hata kutoa moyo wako lakini huwezi kupenda wala kupendwa, huwezi hata kuwa  mbunifu wa kitu chochote.

Hata hutaona  hatua nyingine ya  upekee wako,  unaharibu HATIMA ya maisha  yako.

Ukitaka kuwa mshindi hapa ulimwenguni jizoeze kutafakari,  utakuwa kama unalisha chakula kizuri akili yako , na kama ni matunda mazuri  basi utayapata kwa kuwa umepalilia vizuri  na kuwekea maji kwa wakati. utaona vitru vikiwa vigumu wewe utaona ni rahisi  na wepesi  wa kurekebisha.

kumbuka kwamba  huwezi kupata matokeo kwa muda mmoja , inatakiwa uzoee kufanya hivyo kila siku ndipo utaona  nguvu ya kuwa sawa  . Shamba lililopaliliwa na kuwekwa mbolea  na kumwagiliwa maji  humea vizuri. ndivyo hivyo nawe unatakiwa kujitahidi kupalilia  akili yako na ubongo wako. mafanikio ni lazima.

Masononeko , huzuni , sikitiko humsogeza Mungu karibu.

maoni yako ni muhimu  yatamsaidia mtu fulani katika maisha yake.

 

 

Previous WAKATI MWINGINE UNAHITAJI KUTULIA:
Next NJIA 10 ZA KUMSADIA MTU ANAEPENDA KULA :

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.