NGUVU YA NIA KATIKA KUMTAFUTA MUNGU.


Katika maisha ya kiroho Nia ina mambo mawili, ya kwanza ni Upendo na Kusudi, ya pili ni madhara na maono ya juu. Kila kitu kinategemea na nia.
Kama utaweka nia yako kwa Mungu , roho yako itakua, kama utaweka nia yako kwenye vitu pia itakua kwenye hivyo vitu badala ya Mungu.
Mara utakapopanda mbegu ya nia, safari yako ya kiroho itaendelea vizuri bila kizuizi.
.Msingi wa nia ambayo inaonyesha maisha ya kiroho, inaelezea mafanikio ya mtu anayotaka.

1.Kutaka kuhisi uwepo wa Mungu
Uwepo wa Mungu ni mzuri katika maisha ya mtu,unapoondoka, mtu huhisi kama kutengwa, kubaguliwa,kupata shida, kukosa kazi, migogoro ndani ya ndoa,familia,kila mahali unahisi kutengwa.
Ukiona hivyo ,jitahidi kujiunganisha na familia au makundi yenye kumtafuta mungu wa kweli. Ukifanya hivyo itakusaidia kupata amani, kwa sababu tunahitaji kutosheka haijalishi ni kiasi gani cha kundi unaloendea.

2.Kuhitaji msaada wa Mungu
Uwepo wa Mungu unakuwepo kutokana na sifa ya roho yako, na ni katika vyanzo vyote vya sifa, upendo, Ukweli, Kuwa muwazi, Uzuri wa mungu, Utengenezaji Amani.
Kukua kwa vitu hivi ndani ya maisha yako ni dalili ya kuwa karibu na roho ya Mungu.

3.Kutaka kujisikia kuunganidhwa na kila kitu
Safari ya kiroho inamchukua mtu kutoka katika hali ya chini kabisa kama vile kipande kidogo na kufikia hali ya juu yaani ya uzima.Hii utajisikia kuunganishwa zaidi nae.

4.Kutaka maisha yako yawe na maana
Unapotengwa, unahisi uko sehemu ambayo haina kitu “patupu” katika hali hii utapona tu pale utakapojiunganisha na Mungu. Badala ya kugeuka na kuanza kutafuta kusudi , Rudi kwake utapata ukamilifu.

5.Kutaka kuwa huru kutokana na kizuizi.
Woga ni matokeo ya kutengwa, lakini uhuru wa ndani unaeleweka pale woga unapotokea. Unapokaribia roho ya Mungu, mipaka yote ya zamani huanza kuyeyuka. Badala ya kuogopa kuhusu maisha ya baadae, unakabiliana nayo. Na maisha yako yatasonga kama mto wa maji, bila kusubiri ni lini mipaka ya zamani iliokushika kurudi kwako.
.Nia ambazo hazimtafuti Mungu ni kama hizi.
Nahitaji kushinda
Nataka kujihakikishia kwa kuchukua hatua yoyote
Nataka kutengeneza sheria
Nataka kuwa katika utawala
Nataka kufanya hivi kwa njia zangu zote.
fuatilia mafunzo ya kiroho kila jumapili na utakuwa wa tofauti.

Previous AFYA YA MAHUSIANO.
Next MWONGOZO WA KWELI KATIKA NIA ZETU ZA NDANI

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.