NITAMSAMEHE VIPI MTU ALIENISALITI NA KUNIUMIZA MOYO WANGU.


33978CE600000578-3561746-image-a-15_1461775021115 NITAMSAMEHE VIPI MTU ALIENISALITI NA KUNIUMIZA MOYO WANGU.

Kama hujawahi kuumizwa na mtu fulani, ukaumia ndani kabisa,  inawezekana unatembea na hayo maumivu ndani ya mwili wako-hata kama ilitokea miaka iliopita

.muda huwa hauponyi vidonda  vilivyopo,mpaka ushughulikie tatizo , tunatunza maumivu hayo ndani ya miili yetu. Tunajidanganya kwa kuvifunika vidonda   tukijua kwamba tutapona kwa kuchagua mtu mwingine  wa kukufanya uwe na furaha.

Unapovunjika moyo,  waokoaji wetu hutuambia  tufanye tuwezavyo ili kuachana na  maumivu. Nilipojaribu kuondokana na huzuni ya ndani kutokana na kuumizwa mwanzo, afadhali ningejisikia kukimbia kabisa ili niondokane na maumivu.kwa sababu nilikuwa na nia ya kupona. Nilijua kukimbia   haikuwa  chaguo.

Katika majibu ya maumivu , wengi wetu hukimbia, wengine hujituliza, wengine hujirudisha wenyewe, na wengine hupatwa na hasira. Wengi wetu huumia kwa sababu  huwa hatukubaliani na kilichotokea na kusamehe . jinsi wanavyokuwa na maumivu, uzoefu huu unaweza kutufundisha  mambo mengi yanahusiana  na maisha yetu- na kufanya utaratibu wa kusamehe.

Hapa kuna mambo machache  ya kukumbuka  katika safari yako ya kuachilia .

1.Jisamehe Mwenyewe, Sio Mtu Mwingine.

images-10 NITAMSAMEHE VIPI MTU ALIENISALITI NA KUNIUMIZA MOYO WANGU.

Kukataa kumsamehe mtu  itakuumiza mwenyewe,na sio mtu mwingine. Uwezo wa kusamehe mara ngingi hutokana na shina  lililoko ndani mwako la kuumiza mtu mwngine kama wewe ulivyouumizwa basi utataka  kulipa kisasi, kumuumiza  huyo tena. Inaweza pia ikawa  ni woga  wa kuachilia. Hatua ya kwanza ya kusamehe ni  kujijali  mwenyewe  na kupata nafasi ya kujisamehe.

2.Kila Mtu Anajitahidi Kuwa Bora Kadri Awezavyo.

IMG_0991-840x512 NITAMSAMEHE VIPI MTU ALIENISALITI NA KUNIUMIZA MOYO WANGU.

Haijalishi ni katika hali gani, mtu aliekuumiza  hufanya awezavyo kuwa bora,  wengi wetu  huwa hawamuumizi mtu kwa makusudi , Inatokea’’. Kwa wale wanaokusudia, hufanya hivyo kwa sababu  nao wameumizwa ndani  ya mioyo yao. Kuendelea  kurudi kwenye huu ukweli, msingi wake ni  kusamehe. Inatusaidia kuona ubinadamu wa wale  waliotuathiri  badala ya  kuanza kuwarudishia matendo mabaya. Nilipoumizwa na mtu fulani, sikubali  na sikutaka kuongea , au kuwasema vibaya. Badala yake  nilijaribu kuelewa  kwa nini wameamua  kufanya hivyo. Naamini kwamba  wanafanya  kwa sababu wanataka  kupata kitu kilicho bora kwao na huenda kuna kitu wanakihitaji .

3.Ni wewe Pekee Unaweza Kujidhibiti.

Betrayal_Quotes8 NITAMSAMEHE VIPI MTU ALIENISALITI NA KUNIUMIZA MOYO WANGU.

Tunapokuwa tumeumizwa na mtu mara nyingi tunahisi hatuna nguvu. Tunapokubali huu ukweli, hurudisha lengo  kwetu wenyewe. Mara zote kuna kitu tunachokidhibiti. Jifunze uwezacho  kuhusiana na wewe mwenyewe na ukue. Chagua unataka uwe mtu wa aina gani  badala ya kukazana  na mambo  yanayohusu watu wengine au hali iliopo ambayo huwezi kubadilisha.

4.Huanza Na Kujifunza Kutaka Vitu Vizuri Kwa Ajili Ya Watu Wengine.

Napenda kumtuma upendo na mwanga mtu alieniumiza .unaweza ukafikiria mtu aliesimama mbele yako ,  halafu moyo wako unaachilia upendo , na wao watakupa upendo  pengine hata zaidi  ya ulivyofanya. Ni zoezi zuri la kukusaidia  kukumbuka kwamba upendo  ni  mzuri.kama ukitoa upendo , upendo huo utakurudia zaidi ya ulivyotoa. Upendo wako hauna kipimo.

5.Kuongelea Msamaha Wako Ni Muhimu.

Ninapohitaji kumsamehe mtu ,  huwa nasema hayo maneno kwa sauti mara moja iwezekanavyo. Huwa nawafikiria wao kuwa na furaha  na amani ya kutosha , ambayo ni kitu ambacho kila mwanadamu anakihitaji maishani mwake. Mwanzo utakuwa unapata shida kama umeshikilia bila ya kuachilia msamaha. Lakini ukiachilia, utaanza kuona  rahisi mwenyewe kusamehe, na maneno huja kwa urahisi kutoka mdomoni mwako, utaanza kuona mwanga na moyo wako  utaanza kufunguka kwa kadri unavyoendelea kusema maneno hayo ya msamaha, na utaweza kuachia upendo  kwa mtu aliekuumiza.

6.Upinzani Wa Kusamehe Huja Kutokana Na Kukataa  Kutoa Maumivu.

Mara nyingi nitasema kwa sauti ,  nimekuachilia wewe,( unamtaja jina) ninapoanza kupata ufahamu  kuhusu wao au hali ya maumivu,  nitajiuliza  ingawa  kitu sio cha lazima.kuna sehemu ya afya ya uponyaji   unapoondokana na maumivu,  lakini  hii inaweza ikawa ni majivuno  pale mkanda unapoanza kucheza ndani yako kwa kurudia  rudia yaliopita . jitahidi kuachilia yaliopita, na ukazanie yajayo  unayotahili kuyapata.

7.Ni Mlolongo Mrefu.

Wakati mwingine maumivu huwa yamezidi sana  kiasi kwamba huwezi kufikiria hata namna ya kusamehe. Ni muhimu kukumbuka kwamba  msamaha una mpangilio wake. Kupona  kuna njia zake. Tunafanya utaratibu. Tunafikiria tumesamehewa. Na mara tunakuwa ndani ya maumivu tena. Ni sawa katika kupitiia hali hizo,  Anza  utaratibu  wa kusamehe kila kitu tena. Na uachilie .

Ingawa wakati mwingine  tunaona kuwa ni vema kutoishi na maumivu ,  uzoefu huu ni mzuri, nafasi ya lazima  kwenye maisha yetu tunapokua, tunapoamua kufanya mchakato kuhusu maumivu yetu,  kujiangalia zaidi sisi,  na kuwaachia wale waliotuumiza, tunafanya kitu cha muhimu  katika mabadiliko yetu wenyewe.

 

Toa maoni yako na pia shirikisha na wengine wajifunze.

 

Previous JINSI YA KUWA MWENYE FURAHA NA KUJIFUNZA KUSHIRIKISHA UKWELI ULIOMO NDANI MWAKO
Next RAFIKI ANAEKUJA KWAKO KWA AJILI YA KUTAKA FAIDA YAKE BINAFSI, ATAKUVUNJA MOYO.

2 Comments

  1. […] =Nitamsamehe vipi mtu alienisaliti na kuniumiza moyo wangu […]

  2. […] -Nitamsamehe vipi mtu aliyenisaliti na kuniumiza moyo wangu […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.