Njia 10 Za Kudumisha Upengo Milele


Kuwa na mahusiano ya kudumu sio jambo la kisayansi.

images Njia 10 Za Kudumisha Upengo Milele

kukiwepo Upendo na maelewano, unaweza kutengeneza msingi mzuri ulio imara na kujenga ndoto yako ya baadae.

Hapa kuna baadhi ya njia  zitakazo kusaidia

1.Kila mmoja kuwa ,mwema kwa mwenzake.

Jambo hili ni mtihani kwa wengi, msipojaliana na kuheshimiana , mnapoacha kufanyia mambo mazuri, kufunguliana mlango, kupika chakula kizuri,  na kumwambia mwenzi wako kuwa ”unampenda”

2.Kutafuta vitu vidogo vidogo ambavyo vitamfanya mwenza wako atabasamu 

Mimi huwa ninaita utundu. kila siku unatakiwa uwe unatafuta kitu cha kumfanya mwenza wako atabasamu. kitu ambacho kitamfanya  ajue kuwa ulikuwa unamfikiria.

3.Usipende kuweka mambo moyoni mwako.

Kuweza hali hii ni kukataa tabia ya kulimbikiza makosa yanapotokea, Ongea na mwenzako, kama huwezi kuongea mwandikie vitu vyote ambavyo hukupendezwa navyo kwa siku hio . usisubiri siku ipite na hicho kitu umekishikilia.

4.Msibishane mbele ya Watoto

Zawadi kubwa na iliyo nzuri kwa wazazi kuwapa watoto wao, ni kuwa na mahusiano mazuri, mnapogombana watoto wanapatwa na wasiwasi, na  kamwe msitumie neno talaka mbele yao. italeta sumu masikioni  na mioyoni mwao.

5.Kila siku Angalia ,mazuri ambayo mwenza wako amekufanyia.

Watu wengi huangalia zaidi mabaya badala ya mazuri. Lakini kama utakuwa unampongeza mwenza wako na kumsifia kwa mambo kadhaa italinda ndoa yenu.

6.Kamwe usiwe mtu wa kulaumu,  Kuleta aibu, 

Ni rahisi kumnyoshea mtu kidole, Lakini kabla hujafanya hivyo fikiria kwanza kwa dakika chache, Anza kujiuliza  kitu ambacho unataka kukisema, kitamfanya mwenza wako ajisikie vizuri?  huo ndio ufahamu  utakao kusaidia kuongea kitu kizuri  na kwa njia nzuri.

7.Acha kinoti cha Upendo.

Mwenza anapokutana na kinoti hicho cha upendo, kitamfanya ajisikie vizuri siku nzima, kama ni kazini  au hudumu yoyote atafanya kwa amani na kwa umakini , huku akiwa na hamu ya kukuona mapema.

8.Hakikisha mnaenda Kulala pamoja.

Mshike mwenza wako mkono   mnapotaka kwenda chumbani, sio kila mtu anaingia kivyake.  Jitahidi kuwa na muda wa kukaa pamoja kwa karibu .Kama mwenza wako anataka kulala mapema kabla yako, jitahidi kumsaidia alala na wewe urudi kuendelea na kazi zako.

9. Muwe na wakati wa kukaa mezani kila siku mnapokula chakula cha usiku

Hii ni njia nzuri ya kuwasaidia watoto waje kuwa wazazi wazuri baadae. Kuweza kuwafahamu tabia zao. Pia kumbuka kuwa ni lazima kuwa na muda wa peke yenu kula chakula nje ya nyumba yenu.

10.Amini kuwa upo na Mtu Sahihi.

Ukiwa na shaka kuwa mtu huyo sio mtu sahihi, hutaweka nguvu kubwa ya kuboresha mahusiano yenu.  Lakini ukijiamini kuwa ulichagua kwa busara, utafanikiwa kujenga mahusiano yako kwa ubora mkubwa

Kuna njia nyingi unaweza kufuata, Anza na hizi , Na usijaribu kuzitumia zote kwa mara moja .Anza na namba moja. Halafu zingine zaitafuatia kwa urahisi.

Subscribe.

Previous Lugha Ipi Ya Mapenzi Inayokufaa? Na Mwenza Wako je?
Next Unahitaji Msaada Kwenye Mahusiano Yako?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.