Njia 5 Akili Yako Imekudanganya Wakati Ulipovunjwa Moyo


manbroken Njia 5 Akili Yako Imekudanganya  Wakati Ulipovunjwa Moyo

Ulipovunjwa moyo Akili yako ilikutaka uwe unakumbuka maumivu tu kila wakati.

Maumivu ya hisia ambayo yanatokana na kuvunjika moyo yanasababisha magonjwa makubwa yasiotibika. Kwenye hatua hii huwa hakuna mtu anayehusika, wala kitu chochote.

Wewe mwenyewe unaweza kuzika kazi hiyo , kwa kufikiri, au kwa kuondoka mahali unapoumizwa na kwenda mahali salama kwa muda kwanza. Wakati huo sio vizuri kukaa peke yako kwa kuwa kama utabaki mwenyewe, kila unachoona ni yule mtu aliyekuumiza moyo na kusikia maumivu makali zaidi.

Kitu tunachokihitaji zaidi ni maumivu kutulia au yaondoke kabisa, Lakini hiki sicho ambacho akili zetu hukitaka.

Unapokuwa umevunjika moyo , Akili inakuwa na Agenda tofauti na unachotaka kufanya, matokeo yake huishia kukudanganya na kuyafanya mambo yote kuwa mabaya zaidi.

Kama tukitaka kuepuka  na kuachana na maumivu  ili tusonge mbele , tunahitaji kufahamu  ni wakati gani sio wa Kuamini kile ambacho akili inakuambia.

Kwa Nini Tusiamini Akili zetu Tunapokuwa kwenye Maumivu Ya moyo.

Ili usiumie ni vizuri kama utakubali matokeo ya kuvunjwa  moyo na mtu uliempenda na kuwa na juhudi ya kusonga mbele. Punguza muda uliokuwa unatumia kumfikiria  mtu huyo. kwenye mawazo yako hakikisha unamfuta kidogo kidogo sio mara moja.

5832660048_55f8b0935b_b-1024x685 Njia 5 Akili Yako Imekudanganya  Wakati Ulipovunjwa Moyo

Akili huwa inataka kufanya kitu tofauti, mambo kinyume, inataka umfikirie mtu muda wote, ushikilie maumivu bila ya kusahau nani na kilichosababisha ni kitu gani. Akili inapenda kufikiri hivyo kwa kuwa mara nyingi inataka kukulinda. Mfano kama  maumivu yalisababishwa na moto wa  mkaa, akili itakukumbusha maumivu ya huo moto, kwamba usiguse tena, kuhakikisha unakumbuka jinsi gani maumivu yalikuwa makali. Kwa hiyo akili inafanya kazi ya kukulinda ili usifanye makosa hayo tena. Ni vile vile kwenye maumivu ya kuvunjwa moyo, akili itakukumbusha kila mara ili ufikirie zaidi.

Utakuwa ni mtu wa kufikiria kwamba…

1.Huyo mtu alikuwa bora, hakuna mwingine, hutapata kama yeye.

Utakuwa unakumbuka sifa zake nzuri, mwonekano wake . Hivi vitu vitakuwa vinacheza akilini mwako na kusababisha maumivu makali yasioisha.

2.Mahusiano yalikufanya uwe na furaha kila wakati.

Hapana sio mahusiano , inawezekana ni wewe ulitengeneza hio furaha.

3.Kama ukimpigia simu au kumwandikia ujumbe utajisikia vizuri.

Unakuwa unajiuliza, nipige au nisipige, nimtumie ujumbe au email, vitu hivi vinakuja kwa nguvu. Lakini kumbuka kufanya hivi vitu unaonekana umechanganyikiwa naye na ni muhitaji, utajiumiza mwenyewe.

4.Akili itakuambia kuwa , kuongea na marafiki kuhusu  ex wako utapunguza maumivu

Hapana . hutapunguza. kuongelea hisia za matukio ya maumivu ni kawaida. tena inafaa. kama utafanya hivyo kwa ajili ya kutatua tatizo, au kama unafanya hivyo ili kuthibitisha hisia . Lakini kama utaenda moja kwa moja kuhusu tatizo lako utakutana na maumivu makubwa zaidi.

5.Ni lazima kujua kwa uhakika kwa nini hicho kitu kimetokea.

Kuwa na uelewa kwamba kwa nini hili tatizo limetokea inasaidia .Ingawa , Ni wachache tu ambao wanakuwa wazi na waaminifu kuelezea kitu hicho. Kujaribu kuingia kwenye vichwa vya maex wetu ili kuelewa kwa nini vitu hivi havikufanya kazi ni  shimo la panya. Ni bora kutambua na  kufahamu kuwa Hawakuwa na upendo au  haikuwa chaguo lao, au makosa yamefanyika.

Kubali matokeo ili upone.

Subscribe.

Previous Tofauti Kati Ya Urafiki Wa Kawaida Na Urafiki Wa Kimapenzi
Next Jinsi Ya Kufuta Hofu, Maumivu na Kuzitawala Hisia

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.