NJIA 6 ZA KUKUZA NA KULEA UELEWA KATIKA MAHUSIANO.


2DEAE7DB00000578-3295457-Cognitive_studies_have_shown_that_men_score_significantly_higher-a-121_1446139284737 NJIA 6 ZA KUKUZA NA KULEA  UELEWA KATIKA MAHUSIANO.

Uelewa ni kitu chenye thamani na umuhimu wake ni mkubwa, uelewa unagusa  maeneo mengi  ndani ya maisha yetu.

Na inaonekana ni zaidi ya umuhimu kulingana na mafundisho ya Dalai Lama katika  kitabu chake kilichoandikwa , Emotional Awareness.

Uelewa ni uwezo wa kutambua hisia za mtu mwingine, kutambua ni jinsi gani anavyojisikia , anavyoona , anavyosikia, hata kama ni kwa maumivu au msukumo.Kuwa na uwezo  huo  utakuwa unatembea ndani ya  utaalamu , kuanzia kwenye mapenzi, urafiki,  uzazi mpaka kwenye siasa.

Kutokana na hilo basi , ni hapo wakati mtu anapobadilika kwa muda na kuingia ndani ya hisia za mtu mwingine na yeye kuhisi kama huyo mtu anavyojihisi. Ina maana kuishi ndani ya mtu kwa muda mfupi, kuendelea hivyo bila ya hukumu  . Ina maana kwamba unahisi kile kile au zaidi  ya hicho. Na ni muhimu  kugusa   kila utu  wa mtu  uwe na mabadiliko  na kuwa na tabia  ilio njema.

Ipo tofauti kubwa kati za  hisia ya akili  na hisia za uelewa. Na imeeleweka kuwa uelewa ni kiungo kikubwa   kwa mtu binafsi  na hisia zake. Na sisi ndio vifaa maalumu vinavyowezekana  kwa wale ambao tuko karibu nao, kwa sababu tunapokuwa karibu na  mtu au watu wengine wanakuwa ni sehemu yetu maishani.

Kuwa na Uelewa inakuongoza kuwa na Huruma . kama utakuwa na huruma kwa mtu au watu wengine ,  Hapo kunakuwepo na hitaji la kuwasaidia kulingana na uwezo ulionao na kuwaondoa kutoka katika mahangaiko walio nayo. Wazo hapa ni kwamba hutaweza kuwa na  huruma  binafsi  vinginevyo uwe na Uelwewa wa kutosha kuwa ni kweli wanateseka.

Maana ya hapa ni kwamba , usitoe kwa ajili ya kutaka kujisafisha wewe, au kwa kujionyesha kuwa na wewe unaweza kusaidia , uelewa ni zaidi ya hilo, vinginevyo utakuwa unajidanganya nafsi yako kuwa na wewe unaweza  kusaidia.

Inaumiza kusema hivi lakini,  ni muhimu kwa wale  wenye utaalamu wa kutoa  na kusaidia   wawe na Uelewa. Na hii ni muhimu  kuanzisha mapema ndani ya mahusiano   iwe kama ni mafanikio na matokeo ya  tiba  ya mahusiano.

Kama wanadamu , mara nyingi  tunafungwa katika maisha yetu  na tunasahau kwa urahisi  kitu cha Uelewa ndani yetu. Ufahamu huu unaweza kujifunza  kutoka kwa wale ambao mko karibu na ni washirika, lakini mara nyingi wengi wetu tunahitaji kukumbushwa jinsi ya kuwa na uelewa.

1.Kuwa na ufahamu wa binafsi

Kwa kadri unavyokuwa wazi  kutokana na hisia zako mwenyewe, ndio unavyoweza kufahamu hisia za mwingine.

2.Tambua lugha ya mwili

Mara nyingi tunaweza kusema mengi kuhusu wengine kwa kuwaangalia  kutokana na lugha zao za mwili, angalia usoni,  mikono , inshara  na  tone ya sauti zao.

3.Kuwa msikilizaji mzuri

Ukiwa ni mtu muelewa , lazima uwe ni msikilizaji mzuri kwa wengine  ujue wanakuambia nini,  mpe mtu nafasi ya kujieleza vizuri  bila ya kumuingilia katika maelezo yake.

4.Ondoa kutokuamini na kuhukumu

Wakati unasikiliza hapo ndio ufunguo wa kupata uelewa, na  ni muhimu kutokuhukumu kile mtu anachokuambia .Unapotaka kutatua shida ya mtu , usiwe na shaka  au kuanza kumpa maana nyingine.hapo utakuwa huna huruma na hutaweza kutatua  tatizo alilonalo.

5.Tumia tafakari

Tunapotafakari ni muhimu kuandika , hio pia ni sehemu ya  kuwa mponyaji.  Hii ni njia ya kutambua maumivu ya mtu  na jinsi anavyojisikia. Unaweza kusema kitu kama vile, Inaonyesha haya unayoongea yanaumiza sana.

6.Weka kado maoni yako na thamani yako

Ni muhimu kufanya hivyo ili uweze kuwa makini  kabisa  na  hitaji la huyo mtu.

img_9128 NJIA 6 ZA KUKUZA NA KULEA  UELEWA KATIKA MAHUSIANO.

Endelea kufuatilia makala nyingi zaidi ili uweze kufunguka.

Shirikisha wengi facebook.

Previous SABABU KUBWA ILIOJIFICHA KWA NINI NDOA ZINAVUNJIKA
Next ZAWADI ILIYO NZURI KUPITA ZOTE SIKU YA VALENTINE

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.