NJIA 6 ZA KUJISALIMISHA SIKU YA MAMA DUNIANI:


1408619819_cc6795224c_o-1024x525-1024x525 NJIA 6 ZA KUJISALIMISHA SIKU YA MAMA DUNIANI:

Uko tayari kwa siku hii?  sina maana kuwa upeleke maua au kadi kubwa, nina maana kuwa ni siku ya furaha kwa mama. kuna wengine wengi tu hawana mahusiano mazuri na mama zao, hata hivyo, wadada wengi ndio huwa karibu na mama zao. na wengi wao huishi nao kwa upendo na wengine wanaishi nao basi tu.

Nini basi kinatokea siku ya mama?

Ni siku ambayo unaweza kuikumbuka kwa mambo mengi ambayo mama huwa anapenda na mengine ambayo huwa hapendi,  kuna wamama wengine pia hawana mahusiano mazuri na binti zao , wamekuwa ni wagumu kuwaelewa binti zao , na hawapendi kuwapa nafasi ya kujielezea hisia zao kwao.

hio tabia inaumiza sana.

Lakini ngoja tumweke mtoto ndani ya beseni la maji. na tunafanyaje hapa, kumtoa out of kila kitu katika siku hii.

watoto wa aina ya kike si wagumu kuwapenda , kwa sababu ni wa aina yake. ni mtoto sio mama.

mama ulie nae ndio mama yako , huwezi kupata mwingine hata  kwa dawa, umetokea kwake ndio huyo mwingine sio wa kwako.

kwa maana hio basi hatuwezi kugonga mwamba. lakini watoto wengi wamekuwa na dharau , hata kuonyesha hasira mbele ya mama, na kuona moyoni mwake na hata kutamka kuwa bora usingekuwa mama yangu, sasa hapo sijui mama mwingine angekujaje hapo.

Unaweza kuona mwenyewe kuwa umekuwa si  binti ambae mama yako alitaka uwe, lakini hakuna njia nyingine tena, mama yako ni wajibu wako. lakini sio kwamba una wajibu kwake tu, ni wajibu wako kwako na kwake kwa wakati huo uliopo unaweza kumsaidia.

kwa hio hapa chini nakupa vitu ambavyo unatakiwa kufanya kwa wote, wewe na yeye.

1.JIPONYE.

Kwa jinsi ambavyo tunatakiwa kuyaponya mahusiano yetu  au ya mtu mwingine, inaweza kuwa katika nguvu zetu au wajibu wetu kufanya hivyo, hatuwezi tu kuwaponya wengune , tunatakiwa tupone sisi kwanza, na hii ni hatua nzuri ya kupata mahusiano bora kwa mama, haijalishi yalifikia kiwango gani.

2.SAMEHE.

Mpaka hapo utakaposamehe, kwa sababu umebeba mzigo na hisia nyingi  zinazoumiza akili na mwili wako. samehe. sio kwa sababu ya kufunika siku hii tu ili kuifanya siku iwe nzuri , hapana.

Ni sawa.  si kila kitu afanyacho mama  kikawa ni sawa, unasamehe ili uwe huru kutoka kwenye maumivu na negativity ulizonazo.

3.HESHIMA.

Inawezekana huna heshima na wala haumpendi mama yako, lakini kumbuka mama ana impact  yake kubwa tu katika maisha yako. na hii inatokana na yeye kuwa na hisia mbaya kwako, kutokana na jinsi unavyomchukulia.

lakini kwa sababu anahitaji kuheshimiwa na kupendwa, jaribu kutafuta namna ya kumheshimu mama pale ambapo nunaona kabisa umemkosea heshima, huenda huwezi kupata muda wa kukaa nae hata kidogo, na kama hio ndio sababu , fanya hivyo japo kwa muda mfupi sana kwa upendo.

kama simu inatosha kati yenu kuwasiliana basi fanya hivyo. usipende kuweka matarajio makubwa ya kumfanyia mama, kama vile  parties, zawadi za kadi kubwa, vitu vya thamani , hapana. fanya kile ambacho roho yako itaona kinafaa kwa ajili ya mama.

4.ZAWADI YA  KIMUNGU.

Nenda na zawadi unayoona  kuwa itamfurahisha mama, sio kitu ambacho unafikiria awe nacho, mpe kitu ambacho kitamfanya atabasamu na moyo wako utafurahia.

5.MIMEA SI MAUA.

Maua ni mazuri , lakini kumbuka maua yatakaa muda mfupi sana na kunyaka na kutupwa nje. lakini ukipeleka mmea, ataupanda na kuumwagilia kila siku. na huo utadumu, na kila akiuona atakuwa anakukumbuka na kutabasamu.

6.PICHA YAKE.

Tafuta picha ya zamani ambayo huenda mlipiga pamoja , au kifamilia. akitazama  inamkumbusha , inaweza kuwa wewe ni binti na huenda ikawa mnafanana nae , basi akikumbuka jinsi ulivyo sasa na kipindi yeye alivyokuwa  anafurahi. na inawezekana amefanya mazuri alioweza kufanya  mpaka umefikia  hapo ulipo.

Fanya hio picha iwe ndio kadi yako nzuri kwake, ambayo inakufanya uwe mtoto mzuri kwake.

Siku ya mama, ni siku yake. kwa sababu ni mama yako huyo. lakini siku hii pia ina  mengi ya kufanya kwako kwa sababu. ni vizuri, ni mama yako.

Na unaweza kuifanya iwe  siku nzuri kwenu wote.

Previous MASWALI MAZURI 50 YA KUMUULIZA PARTNER WAKO SIKU YA MTOKO:
Next HATUA RAHISI 10 ZA KUFANYA MAZOEZI YA MEDITATION:

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.