Njia 7 Za Kujifanyia Wema Wakati Upendo Wa Kipekee Hauji Kwa Urahisi


self-care-3-1024x512 Njia 7 Za Kujifanyia Wema Wakati Upendo Wa Kipekee Hauji Kwa Urahisi

Hivi karibuni nilikuwa kwenye maendeleo ya kujifunza jinsi ya kuwa na mahusiano mazuri  na mimi mwenyewe.  Jitihada  hizo  ni za kuhisi kutopendwa na kutojithamini.Mara nyingi jitihadi za kujipenda ni ngumu  kuendeleza. Nashukuru niligundua  njia : Kujihurumia

Kwa kujifanyia huruma kidogo  kwenye njia hizo , nimeweza kutambua upendo wa kipekee unakuja kwangu, naendelea kulea  zaidi , mahusiano yangu binafsi . Hapa kuna matendo ya huruma  ambayo niliweza kufuata kwenye jitihada zangu za kupata upendo wangu mwenyewe.

1.Fikiria Wema Kwa Ajili Yako

Umewahi kusikiliza mawazo yanayozunguka ndani yako?  mengi sio ya kupongeza.  mengi ni ya kujilaumu. mengi  kamwe sio ya kwetu. Na hutaweza kuongea kwa mtu mwingine  jinsi unavyoongea kwa ajili yako. kwa hio kwa nini usiingize huruma kidogo kwa ajili yako kwa njia hio. Unafanya mazuri na hayo mazuri yanakutosha.jipende kwa kujisemea   maneno mazuri , fanya wema kwa ajili yako.

2.Jisamehe Mwenyewe

Kila mtu hufanya makosa, mara nyingi,  sio wote ambao wanaweza kusamehe kwa urahisi wengine au kujisamehe wenyewe kwa urahisi, kwa makosa hayo.  Kwenye huruma ni kuwa na uwezo wa kusamehe  yale mabaya tuliyoyafanya au yalio kinyume nasi. Kama wewe ni mmoja wa wale wanaoshikilia makosa,  huenda unahangaika katika kusamehe na kujisamehe. Ruhusu  huruma iingie ndani yako.  kujipenda ina maana  ni kujipenda hata unapokuwa na makosa . kitu ambacho kila mtu hufanya wakati kwa wakati.

3.Jilinde mwenyewe.

Maisha mara nyingi hayawi kama unavyotaka. wakati mwingine unaona kama maisha  hayana wema. Utabaki ukishangaa  kwa kuona maumivu  na kuvunjwa moyo  kwenye Dunia hii. Nyakati hizo zinapokuja , jilinde mwenyewe. ruhusu kusikia hisia zozote zinazokuja. Iwe ni woga, Hasira, Maumivu, Kukatishwa tamaa, Pata muda wako wa kushughulikia bila ya kujilaumu au kulaumu mtu mwingine kwa kufanya makosa.  Jipende kwa kujiwekea ulinzi wako.

4.Jikumbatie mwenyewe.

o-HUGGING-YOURSELF-570 Njia 7 Za Kujifanyia Wema Wakati Upendo Wa Kipekee Hauji Kwa Urahisi
hug yourself

Zungusha mikono yako kwa upendo kama vile unamkumbatia mtu mwingine, lakini ni wewe. achilia upole ndani yako. jikumbatie kama unamkumbatia mtu mwenye  huzuni  au ambaye anasikia upweke au kuvunjwa moyo.  mahali ambapo hakuna mtu wa kuku hug. usifanye kama unampa upendo huo mtu mwingine, jipe wewe.  zungusha mikono yako na ujipende mwenyewe.

5.Jipende mwenyewe.

Sasa kabilia na hili.  Ni mzuri, una furaha kwa kila kitu, kwa hio , kwa nini unajifungia ndani , unanunua vyakula hotelini na kupeleka kula nyumbani ukiwa umevaa pajama zako?  Ni wakati wa kuondoka hapo kwenye kochi lako tena. Sio na mtu fulani, bali ni wewe peke yako. Nenda mahali pazuri ukapate lunch  au dinner, kama utajisikia vizuri.  Agiza kinywaji unachokipenda.  furahia. huko ni kujipenda mwenyewe. sio kutegemea mtu mwingine akupende kwa namna hio.

6.Cheka Ukiwa Mwenyewe.

relaxing-1024x512 Njia 7 Za Kujifanyia Wema Wakati Upendo Wa Kipekee Hauji Kwa Urahisi

Fikiria ni lini ulicheka kwa nguvu? baadhi watasema siku iliopita, lakini wengi hawakumbuki. hio ni kwa sababu hakuna kitu kizuri kimetokea kwetu .  tumekuwa  na mambo mengi . kwa sababu ya kukua kwetu.  kwa kadri unavyozidi kukua na kucheka kunapungua. Lakini hii sio kweli . Tafuta kitu cha kukufurahisha na utaweza kucheka kwa nguvu . kujipenda ina maana ni kucheka mwenyewe wakati mwingine, acha wafikirie kuwa una kichaa. lakini una akili zako.

7.Sherehekea mwenyewe.

Ni lini uliwahi kufurahia kuishi kwako?  sio tu kwa ajili ya mafanikio na kukamilisha  jambo. lakini ni kwa kila ulichonacho katika maisha yako. maisha sio rahisi kila wakati.  inahitaji moyo kuwa imara  nyakati ngumu.inahitaji ujasiri wa kusimama tena baada ya kuanguka.  inahitaji nguvu mpya ya kuonekana tena  baada ya kushindwa.  Lakini umefanya hivyo nyakati kwa nyakati tena. kwa hio unasubiri nini? Kujipenda kwa kusherehekea  yote ambayo umefanya, lakini cha muhimu zaidi, ni vyote ulivyovumilia vifurahie.

Kama umependa makala hii, washirikishe na wengine.

Previous Picha Haiwezi Kuonyesha Huzuni Ilivyo,Kwa Sababu Huzuni Ni Kitu Kisichoonekana
Next Dalili Za Uamusho Wa Kiroho.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.