Njia Rahisi Ya Kuondoa Tabia Mbaya Usizozipenda


 

 

Badilika

Wala msifuatishe namna ya Dunia hii, Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu .

1.Anza kujifikiria wewe mwenyewe kwanza ni tabia gani unayoitaka na ipi huitaki, Unao uwezo mkubwa ndani yako, ila hujajua kuutumia.

Hapo Mwanzo Mungu aliziumba Mbingu Na Nchi, Nayo Nchi ilikuwa Ukiwa, Utupu Na Giza lilikuwa juu ya uso  wa vilindi vya maji.Roho ya Mungu ikatulia juu ya maji, Mungu akasema  iwe Nuru , Ikawa Nuru.

2.Rudia Rudia Tabia unayoitaka  na itakuwa ya kwako. kama vile Yoshua alivyoambiwa , kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku. Yoshua  1:8

Tabia nzuri ni ngumu kuitengeneza lakini ni rahisi kuiishi.  Tabia mbaya ni rahisi kuitengeneza lakini ni ngumu sana kuiishi.

How-to-Break-Bad-Habits-1 Njia Rahisi Ya Kuondoa Tabia Mbaya Usizozipenda

3.Ukiamka Asubuhi kila siku sema asante Mungu, Kwa wema wako, Asante kwa Upendo, Asante kwa mafanikio, Asante kwa vitu ambavyo tayari ninavyo.

Shukuruni kwa Kila Jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika kristo. 1Wathesalonike 5:18

Siri ya mafanikio yako inategemea Agenda yako, utakavyokuwa kesho fanya leo. uwe na lengo la siku, wiki, mwezi, mwaka, miaka.

4.Ukitaka kufanikiwa kuwa na tabia njema au kitu kingine chochote , utahitaji NIDHAMU na Kukipenda kitu unachokitaka. Unatakiwa ufanye kila siku kila siku. sio leo unafanya , kesho hufanyi, hutaweza kufanikiwa. sema haya maneno kila siku kila wakati . Muombe Mungu akupe Upendo, Furaha, Amani, Utu wema, Uvumilivu, Fadhili, Upole , Uaminifu na Nidhamu.

Vitatokea kwako.

5. Nidhamu sio adhabu, bali ni rafiki wa kweli anayekulinda na kukufundisha . badilisha mtazamo wako. Jifikirie kama mwanafunzi kila siku  kama unataka mabadiliko.

Kila kitu kizuri unachokitaka unaweza kupata ni uchaguzi na maamuzi yako. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana. Dunia na wote wakaao ndani mwake. Unataka mahusiano mazuri, kazi nzuri, Biashara nzuri, amani na utulivu. utapata ukiamua .

break-bad-habits Njia Rahisi Ya Kuondoa Tabia Mbaya Usizozipenda

Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana yeye ndiye akupaye nguvu za kubadilika . ili uwe na tabia nzuri  uachane na tabia usiyoitaka , Mkumbuke Mungu , Mkubali Yesu .

Subscribe  kupata makala mpya.

Previous Siri Kubwa Za Mafanikio Kwenye Ndoa, Mapenzi, Kazi, Biashara
Next Ndoa Inayobebeka Ni Ipi Nyakati Hizi

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.