Pambana Na Nguvu Inayozuia Unabii Wako Kukamilika


Kuna vitu ambavyo vinazuia Unabii wako usitimie , Lakini nakuambia Kuwa upo uwezekano . Unabii wako lazima utimie. 

IHOP_singer Pambana Na Nguvu Inayozuia Unabii Wako Kukamilika

Zipo sauti mbaya zinakusemesha ndani yako kuwa hutaweza kitu. Hio sauti ndio adui yako , kataa hio sauti. Kuona watu wengine wanaweza wewe huwezi  sio kweli, unaweza . Sauti hio inakutisha, inakuogopesha, inakuambia hutapata kazi kwa kuwa huna vyeti, huna sifa za kuajiriwa, Inakukatisha tamaa.

Usikubali kuchelewesha unabii wako kutimia kwa sababu ya kusikiliza sauti hio.  muujiza wako uko karibu. kabiliana na tatizo lililo mbele yako , hilo tatizo ndio ngazi ya kukufikisha kwenye muujiza wako. Unayo silaha ndani yako mwenyewe, usitafute silaha ya nje. Tengeneza ndani mwako . Kumbuka mawazo ni kama mawimbi  yanapita, ukiyaruhusu tu yanakaa kwako . hizo sauti ukizikataa zinakuacha. Sauti za kuwa wewe hufai. mbaya, huna thamani, sio kweli. Geuza hayo maneno unayosikia yawe kinyume chake .

Ukisikia ndani huwezi Sema unaweza. Ukisikia ndani unaambiwa mbaya, sema wewe mzuri , wa thamani, unastahili.  Pambana na hio sauti yako ya ndani. Usipokabiliana na hali yako ya ndani hutakuwa na uwezo wa kukabiliana na hali yako ya nje.

Sauti inayokuambia kuwa hutapona , kataa sema Yesu alikufa kwa ajili yako, kwa kupigwa kwake umepona. Ukiona Hofu , Kataa sema hatukuumbiwa Roho ya hofu bali ya ujasiri.  Ukisikia Aibu  ikatae hio hali, sema ninayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu.  Huzuni kataa, iambie huzuni nenda kuzimu, huna nafasi kwangu. Kataa mahusiano mabaya, hakuna mahusiano mabaya kama unampenda Mungu  huwezi kushindwa kwenye mahusiano.

Wewe ni Mzabibu unaochanua , kamata wale mbweha wote watupe nje wasiharibu  mzabibu wako. pigana na kila aina ya kizuizi.

Kitu Gani Cha Kuzingatia.

1.Acha Kunung’unika.

Uwe makini na tabia ya kunungu’unika kwa sababu utazuia miujiza yako yote, Unabii wako hautakamilika  mapema. mwili ukiwa dhaifu ina maana maneno yako si kitu, jinsi maneno yako yalivyo ndivyo matendo yako yalivyo. uwe na nia ya KRISTO. Nia safi.

2.Kuwa makini na Huzuni.

Ukiwa na huzuni tambua kuwa akili yako imeumia. Huzuni ni kujikataa mwenyewe kutokana na kupoteza kitu au kuondokewa na mtu wa karibu sana, au kupotelewa na kitu cha thamani sana. Huzuni ni kitu cha muda mrefu, itakukosesha furaha kabisa .Dalili za Huzuni ni hizi

Kukosa usingizi

Kujitenga na watu

Inakupiga upofu usione Neema ya Mungu maishani mwako

3. Hisia za kukosa matumaini.

Utaanza kujihisi kama umepotea, umepoteza muda , hupendwi, huthaminiwi, hutaweza kitu chochote, hakuna Mungu. maana hupati majibu ya maswali yako.

Nakaka nikupe habari njema Endelea kumshukuru Mungu, furahia uweponi mwa Mungu kila wakati, mkumbuke Mungu kila wakati, Msifu Mungu, Usijilinganishe na mtu yeyote. Tumia Muda wako vizuri. usiache nafasi ndani yako kuwaza kitu kibaya. iweke Akili yako bize. Soma neno , ukichoka andika kitu, ukichoka chora kitu, ukichoka fanya kitu kizuri kwa wengine kwa kuwasaidia. Kama upo nyumbani fanya usafi wa nyumba , buni kitu chochote cha kufanya hapo nyumbani usikae bila kufanya kitu. Hio mibweha midogo midogo itakuacha , itatafuta mahali kwingine. Utakuwa Salama.

Unabii wako utaanza kukamilika, Miujiza utaanza kuiona.

Subscribe kupata makala mpya nzuri kila siku.

 

Previous Unahisi Umefungwa Kwenye Mahusiano Mabaya?
Next Maana Ya Maisha Huenda Ni Maisha Yenyewe

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.