Sababu 4 Mazoezi Ya Cardio Yanahujumu Lengo La Uzito Wako


homeworkout_feature3-1024x703 Sababu 4 Mazoezi Ya Cardio Yanahujumu Lengo La Uzito Wako

Kabla hujafikiria  kuwa mwili wako  unashambuliwa  na sakata la kupungukia baadhi ya nguvu,  ngoja nikuambie kuwa  Aerobic ni mazoezi mazuri kupita aina nyingine  kwa ajili ya mwili wako.

Kwa nini nasema hivyo, kwa sababu  yanaboresha  afya ya moyo na kuongeza  uwezo wako wa mapafu kupumua vizuri  kwa muda mrefu, usiache zoezi la cardio moja kwa moja . lakini kwa kusema hivyo  pia cardio inasaidia  kushape mwili wako na  kupunguza uzito.

Kama mazoezi yako ni ya kukimbia  au kupanda mlima  au kuendesha baiskeli kwa nia ya kupunguza uzito, utakuwa umeseti  mpango wa kushindwa kupungua. Hapa ni kwa nini:

1.Diet yako Inabidi iwe ya muhimu

Kupungua uzito, Hata hivyo, huja kwa ajili ya ya kubalance nguvu.kupata calories   katika kinyume cha kutoa calories. Miili yetu inatumia nguvu katika njia tatu: Ya kwanza ni kupitia kupumzisha metabolism, ambazo unaziunguza unapokuwa umefanya kazi nyingi , hasa mwili unapofanya nzito. hio ni katika kupumua na mapigo ya moyo kufanya kazi ya msingi.Ya pili ni thermic effect ya chakula. ambacho kinaunguza kile unachokula. Na mwisho ni kazi za kimwili ambazo huchukua kama dakika 15 au  mpaka 25 tu  kuchoma calories.

Kwa hio ukitazama kwa karibu utaona jinsi ambavyo unaunguza  calories nyingi kuliko ambazo unaingiza . kwa namna hio mpango wako wa  au lengo lako halitafanikiwa. lakini ambacho unakiingiza ndani ni juu yako.

2.Mafunzo ya kunyanyua uzito ni njia nzuri zaidi  ya ufanisi kwa ajili ya kupunguza uzito na kujenga mwili.

hate-the-gym-but-want-to-lose-10-pounds-try-this-simple-at-home-workout Sababu 4 Mazoezi Ya Cardio Yanahujumu Lengo La Uzito Wako

Kufanya mazoezi ya kunyanyua uzito angalau mara mbili au tatu kwa wiki  ni njia nzuri  . Na kwa sababu nzuri  pia . fikiria kuhusu mafunzo ya upinzani kama mtu kufundishwa kuvua samaki. ngoja nielezee kidogo.

Kukimbia kwa dakika 30 utaweza kupoteza calories 200, wakati kama ukifanya mazoezi ya kuinua uzito  kwa muda wa chini ya hapo utapoteza calories kama  hizo. na utapata faida zaidi kama kujenga misuli.

Kwa hio unapofanya zoezi la cardio  ni kama mtu anayevua samaki. , kunyanyua uzito  ni kumfundisha mtu kuvua samaki.  kwa maneno mengine  mafunzo ya upinzani  yanabadilisha mwili wako  kuwa  kwenye hali ya juu katika kuchoma  calories nyingi siku nzima. Iwe ni kwenye gym au nyumbani kwako.

3.Kufanya cardio peke yake inaweza kuathiri maisha yako  yote katika njia negative.

women-in-a-fitness-class-587fa32e5f9b584db3e1a445 Sababu 4 Mazoezi Ya Cardio Yanahujumu Lengo La Uzito Wako

Ukiwa unafanya cardio kila siku , utakuwa unasikia njaa sana kila wakati, na utaanza kusikia hamu ya kula vyakula vya sukari, kwa sababu ya kupoteza calories nyingi kupita kiasi chake.  Na kwa sababu hio hutaweza kupungua uzito kutokana na lengo lako.  Na sasa utakuwa unapoteza na kuongeza , utajikuta unaongeza zaidi wakati mwingine kwa sababu mwili wako utakuwa unahitaji chakula cha kutosha.  Kitu cha msingi ni kuwa na mlo kamili . Kama hutaweza kupata mlo kamili Utapoteza nguvu nyingi bila faida ulioitaka.

4.Shughuli za kimwili haziwezi kubagua

Wachunguzi wameona kuwa  kufanya vitu vidogo vidogo vya kila siku , hata kama unapanda ngazi kila siku na kushuka au kutembea kwa mwendo wa dakika 30, inaweza kuwa na matokeo  mazuri zaidi kuliko mazoezi ya kisasa.

Na kama lengo lako   ni kuweka uzito wako vizuri , inabidi ufikirie mara mbili kuhusu kufanya zoezi la cardio. na badala yake  anza kuongeza  zoezi la kunyanyua uzito ,  uwe na diet nzuri na fikiria  na kazi zako za kila siku zikoje. ni vizuri ukisawazisha  , ni sehemu muhimu  ya kuweka uzito ulio sawa.

Kumbuka kupata vitamini  B12, pata kahawa, mboga za majani za kutosha, coconut water,. Pia hakikisha unapata  chakula kinachofaa kabla ya zoezi  ili kupata matokeo mazuri.

Kama huna vile vifaa vya kunyanyua, unaweza kujitengenezea chupa za maji ya lita moja na nusu, ukajaza mchanga . itakusaidia katika kukaza mwili wako , hasa kina mama wanaofanya mazoezi nyumbani. kwa wanaume wanaweza kutngeneza uzito wa kuzidi hizo chupa. tengeneza uzito unaosawazisha pande zote.  huu ni ushauri wangu, unaweza kuchukua . Na ukakusaidia bila gharama yoyote.

Toa maoni yako kusaidia wengine . kisha usisahau  kubonyeza neno  Subscribe kulia kwako.Ili kupata makala mpya kila siku.

 

Previous Jinsi Ya Kulea Ukuaji Wa Kiroho
Next Huenda Ikawa Maisha Yako Hayaendi Njia Yako Lakini Yanaenda Njia Ya Mungu ( Na Hio Ni Nzuri Zaidi)

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.