SABABU AMBAYO HUJAWAHI KUSIKIA KWA NINI NI MUHIMU WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI


download86 SABABU AMBAYO HUJAWAHI KUSIKIA KWA NINI NI MUHIMU WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI

Ni kuhusu  faida za ubunifu ambao  wanawake wanatakiwa kufanya –kwa sababu wanawake wengi wanakosa  njia hizo za ubunifu.

Wanawake wengi wanakuwa hawako huru kutokana na maumbo yao , na uzito walio nao ni sababu kubwa ya kuwa na hofu ya kukosa baadhi ya  mahitaji yao. Mara nyingi kujihisi kuwa hawako imara, hawana nguvu, lakini hakuna woga kama huu wa uzito , ukweli ni kwamba  mafunzo ya mazoezi yanasaidia kwa kiasi kikubwa kwa wanawake na wanaume kuwa na maumbo mazuri na kujiamini.

Mafunzo mazuri ni yale ya kuwekea nia na kufanya maamuzi  muhimu ya kwamba ni lazima ufanye mazoezi, nimeona watu wengi wakitembea na wengine wakienda gym miaka na miaka , wako vizuri na hawachoki kwenda gym kila siku. Na wanawake ambao wanafanya mazoezi wana nguvu  na ujasiri  wa kutosha.

Na hapa kuna sababu  ya kila mwanamke ni  lazima afanye mazoezi.

1.Utaondoa mafuta  yasiohitajika mwilini

Kwa kuendelea kufanya mazoezi kila siku  au  unaweza ukawa unaruka siku moja moja , mwili wako utaanza  kuunguza mafuta yasio na lazima mwilini mwako kwa kila hatua unayoendea.

Sahau kabisa kusikia kuwa utakuwa na misuli , sijui mihogo ,  hakuna kitu kama hicho, miili ya wanawake ambao wanakuwa na misuli mikubwa ni wale ambao huwa wanahitaji maumbo yao yawe hivyo , kwa maana kuwa hata kama utaamua kunyanyua vyuma, yapo mafunzo hayo na utaweza kuwa na umbo zuri. Kumbuka kwa kila hitaji na nia ulionayo hivyo ndivyo utakavyokuwa.

2.Utakuwa ni mwenye nguvu

Mazoezi yatakuwezesha kupata mwili wenye nguvu, utaepuka na madhara mengi, ikiwa na maana kwamba mazoezi ya kila siku, achana na kutumia dawa za kupunguza uzito. Fanya mazoezi.

3.your butt will tone up

Hutaweza kutumia madawa hapa ya kuongeza umbo lako . lakini mazoezi yataleta umbo zuri la kupendeza na la miujiza ambalo hujawahi kufikiria, mikono itakaa vizuri, miguu yako , makalio , mwili mzima kwa ujumla. Mazoezi yana faida sana , achana na umbo tu  hata kwenye Sex utakuwa tofauti na ulivyo sasa.

4.Kimetaboliki chako kitaongezeka

Mazoezi yanaongeza metabolism, na matokeo yake hudumu kwa muda wa masaa 24 baada ya kumaliza mazoezi, ina maana  calories nyingi  zitakuwa zimetumika , na ukumbuke kwa kadri unavyozidi kufanya mazoezi, mwili wako unakuwa unauunguza calories zaidi kama kawaida, sasa kwa kuendelea kwa muda mrefu  uzito wako utapungua wenyewe kawaida kabisa bila ya dawa.

5.Mifupa yako itakuwa Imara

Kadri unavyokua, mifupa huanza kuchoka, pia wanawake ni mara nne zaidi ya wanaume, kwa hio mazoezi yanajenga mifupa, hutalalamika kuumwa miguu , mara mgongo, ukiwa unafanya mazoezi. Nakushauri dada, mama  fanya mazoezi , hata mara mbili au tatu kwa wiki ili kuimarisha mifupa yako.

6.Mazoezi yatakusaidia kupambana na magonjwa ya moyo.

Mazoezi hayasaidii tu kuimaisha mifupa , bali husaidia kupambana na magonjwa ya moyo . kama unasumbuliwa na moyo kuwa mkubwa, kujaa mafuta , anza leo mazoezi , na kama hujui utafanyaje  tafadhali unaweza kutuma ujumbe wako ili niweze kukusaidia . epuka kupata  mshituko wa moyo, anza mazoezi.

7.Mazoezi yatakupa furaha.

Haijalishi una umri gani sasa, mwanzo ndio huu , anza leo. Utafanikisha mambo mengi tu  kwa kupitia haya mazoezi, yatakupa  furaha ya kipekee na kuwa mwenye amani tele.

Kumbuka kuwa hutaweza kupata matokeo kwa haraka, lazima kuwa na kipindi , kwa kuwa kila unachopanda ni lazima kiote , kwa sababu utakuwa umepanda kwenye udongo mzuri na hewa safi na unamwagilia maji .Amini hilo na utaona matokeo yake haraka tu.

8.Mazoezi Yanaimarisha akili

Faida nyingine kubwa ni kuimarisha akili, unaona ni jinsi gani ilivyo  ukianza kufanya mazoezi, akili yako itaimarika, itakuwa na afya, utaweza kufikiria tofauti, utaweza kuamua tofauti na ulivyo sasa. Utaweza hata kuiweka familia yako vizuri , kutokana na mazoezo  akili yako itakuwa na utulivu.

Ni chakula cha akili, yanasukuma hali  mbaya kuwa nzuri, kujiwekea maamuzi  utaweza kupata uzoefu huu mzuri.

9.Ujasiri Utaongezeka

Akili yenye nguvu na mwili wenye nguvu   husaidiana,  na hivyo  huongeza ujasiri  kawaida kabisa. Mazoezi yanakuletea sababu nyingi  nzuri kuhusu mwenyewe,  kuwa na afya, kuwa mwenye nguvu, kupunguza athari ya magonjwa na kufikia malengo yako ya mazoezi.

10.Hutakuwa  Unaumia umia bila sababu

Ukiwa unafanya mazoezi , nafasi ya kuumia umia haitakuwepo, uchovu hautakuwepo, hii ni kwa sababu misuli yako na mwili mzima utakuwa na nguvu.

Unasubiri nini  Anza leo kufanya mazoezi.

Umeipenda hii makala? shirikisha wengine facebook

 

Previous INATOKEA NINI UNAPOONA UMEFANYA KITU KIZURI ZAIDI
Next KWA NINI DIET SIO NJIA YA KUPUNGUZA UZITO KWA WENGI

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.