Sheria Ya Upendo


look-of-love-teaser-1024x576 Sheria Ya UpendoMsukumo wa kufikia hatima ya maisha yako ni  tumaini, Imani na Upendo.

Lakini ni Upendo pekee una ukweli wa kuwezesha haya yote. 

Haya sasa inadumu imani , tumaini,upendo lakini katika  hayo lililo kuu ni Upendo.

Mara nyingi sana watu hawajali ni kitu gani unakifahamu , mpaka hapo utakapo onyesha  ni kiasi gani  unajali.

Unapotoa kitu fulani kama kufundisha au kuhudumia chochote, jaribu kuangalia sana watu ambao wanaonekana kukosa furaha  au kutokuelewa unachokifanya. Halafu jitahidi kuongea na hao watu ili kujua tatizo walilonalo ili uweze kuwasaidia haraka

Kama utakuwa unahudumia watu kwa kuwapenda na kuwahurumia  hutaweza kukosa mafanikio katika kazi yako, biashara yako, huduma yako.

maxresdefault-1-1024x576 Sheria Ya UpendoKila mara tanguliza Upendo wenye kuhurumia watu. usifanye kitu kwa kutaka pesa, Yaani kuona pesa kwa watu ni mbaya katika maisha. Jambo la ,msingi jaribu kumuona Mungu kwa watu sio pesa. Watu wengi sana huwa wanakosea  sehemu hio, ndio maana ni ngumu sana kufanikiwa.

Fuata  niia za Yesu. Kila alipokuwa akipita barabarani  aliwahurumia watu , aliona jinsi gani wamekuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji . wametawanyika. akawahudumia. wengine wakaponywa.

Moyo wako ukiwa na huruma , utaanza kufanya miujiza kwenye mikono yako. kila kazi utakayoifanya itafanikiwa  . hutatumia nguvu nyingi, bali utatumia maarifa  kidogo  tu , kutokana na ufahamu utakaokuwa nao, kazi zako zitakuwa bora na zenye manufaa makubwa.

Upendo sio zawadi , lakini ni uchaguzi. Ni uchaguzi wa busara.  Achilia huruma ikae ndani ya moyo wako. Upendo ni uchaguzi.

Kiwango unachompenda Mungu, ndivyo unavyofanikiwa kwa kiwango kikubwa  kwenye maisha yako.

Kwa kiwango unachowapenda watu , ndivyo utakavyofanikiwa kwenye kazi, biasharta, huduma yako.

Huwezi kwenda popote bila Upendo. Huwezi kufanikiwa bila Upendo. Upendo ni tunda gumu Ambalo linaliwa kila kitu bila ya kubakiza mbegu au ganda .

Kama hujui niulize nitakuelezea nini mama ya tunda gumu.

SUBSCRIBE.

Previous Kuona Vitu Ambavyo Havionekani
Next Fahamu Mbinu 5 Za Kumwabudu Mungu?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.