Sielewi Kwa Nini Umeacha Kunitumia Ujumbe


 

Sielewi kwa nini umeacha kumitumia ujumbe mzuri , huenda una hisia tofauti si kama nilizonazo  kuhusu wewe, Lakini ninapata ugumu wa kuamini kuwa ni lini mahusiano yetu yatapata nguvu.

Tulipokuwa tukiwasiliana Maongezi yetu hayakuweza kwisha haraka, yalichukua masaa .

Ulionyesha kama una hisia za kweli kwangu. Ulikuwa ukinipongeza. Ulikuwa unaniambia umenimisi. Ulinifanya nijisikie mtu muhimu kwako.

Sasa haupo tena kwenye Ulimwengu huo, Sipati jibu, Siwezi kuacha kujiuuliza maswali ni kitu gani kimetokea kati yetu.

Hatukuwahi kugombana. Sijakufanyia kitu kibaya cha kukufanya usionekane tena. Sijafanya ,siwezi kufikiri nimefanya kitu kibaya.

Huenda ujasiri wangu ndio umekukimbiza, umeogopa. Au sikuweza kukuonyesha hisia zangu zote ukafikiri sikuwa na muda na wewe.

Siwezi kusema ni lini umeacha kunitumia ujumbe, kwa sababu imetokea sasa.

Siku zingine , mambo yanakuwa mazuri. Siku nyingine huonekani tena.

black-woman-smiling-texting-bed-home-47558971 Sielewi Kwa Nini Umeacha Kunitumia Ujumbe

Nimekuwa nikirudia  kusoma ujumbe uliopita ili kuhakikisha kama kuna kitu kibaya nimekiandika, lakini hakuna .

Sifahamu kwa nini umeacha kunitumia ujumbe, kwa sababu tulikuwa vizuri. Nilifikiri tunaelekea kwenye mahusiano ya kweli. Nilifikiri tu marafiki wa kweli. Nilifikiri umeniamini. Nilifikiri nimekuwa karibu na wewe kiasi cha kutaka kuanzisha nguvu kubwa ya mahusiano.

Sikufanya kitu kibaya, Nilikufanyia kila kitu vizuri, Sikuuliza kitu ulipokuwa hujatuma ujumbe. Sikukuchosha na maneno mengi, niliheshimu mipaka yako.

Nimekuwa nikijipa moyo mwenyewe kuwa kupotea kwako ni kwa muda tu. Kwamba utarudi tena. Kila nikisikia mlio wa ujumbe nafikiri ni wewe lakini sio.

Nataka niamini kwamba umepoteza simu au imevunjika. Na kwamba unatafuta nyingine. Kwamba kulikuwa na dharura kwenye familia na hujaweza kunijulisha. Lakini muda wote huo hizi kwamba, labda hazijafanya kazi. Hazina sababu hata kidogo.

Nimetambua sasa. Sielewi ni kwa nini .Hunipendi kama mimi ninavyokupenda.

Huenda uliboreka, au umepata mwingine, aliye bora zaidi. huenda wakati unanitumia mimi ujumbe ulikuwa huna mtu wa kuchat naye, ulijisikia mpweke na ulikuwa umechanganyikiwa. Huenda maongezi yangu hayakuwa na maana kwako kama yalivyokuwa ya maana kwangu.

Sijaelewa kwa nini umeacha kunitumia ujumbe , Lakini nitakubaliana na hali hii. Sitapigania hilo tena. Sitakubembeleza ili uwe katika maisha yangu. Hapana.

Subscribe.

 

Previous Mapenzi Sio Ya Mara Kwa Mara
Next Jikung'ute Mavumbi Uondoke

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.