SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE


4d720edad11df32b2f8ff5451f57b5a1-1024x683 SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE

2017,Wanawake wamepata mwamko zaidi kuhusu afya zao , kuliko miaka ya nyuma, kutoka mwanamke mmoja hadi kwenda kusaidia wanawake wengine, inaonyesha wazi wanawake hawa  wanafanya dunia iwe na  watu wenye afya nzuri.,

kwa kuheshimu siku ya wanawake duniani nakuletea baadhi ya wanawwake ambao  wameonyesha moyo huo  kwa njia moja au nyingine, tunaweza kutamani mambo ambayo wameyafanya. Ni wanawake wa kupongezwa  kwa  uwezeshaji wao .

1.Madeline Albright.  

images-4 SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE

 Sauti yake  ni kutaka kuvunja kila aina ya vikwazo  vya ndani na nje , ni mwanamke wa kwanza  kuwa kwenye hali hio.  Alikuwa na sauti yenye nguvu, ni mtu wa kuigwa na watu, mchapa kazi. Moja ya mistari yake aliyopenda kusema ni kuwa, ilinichukua muda mrefu kuendeleza sauti yangu , na sasa ninayo, sitanyamaza, kwa sababu  ni nafasi yangu kama mwanamke  kwa wanawake wengi.

2.Anne Frank

2017,  Sitaki kuishi kama nilivyokuwa naishi miaka ya nyuma, maisha ya watu wengi ambayo yamekuwa ya kawaida kila siku.  Nataka kutumikia watu , hasa wanawake  , wafahamu furaha ni nini katika maisha , napenda niishi hata  baada ya  kufa.  Kuishi na Nia kama hii  ya kutamani malengo sio pesa, au utajiri; lakini kwa nia ya  kuishi maisha  yanayostahili  na yenye kukamilika. Na kuacha urithi kwa  wengine  kuendelea kuhamasisha  kufikia hatua ya pumzi ya mwisho. Maneno haya alisema Anne Frank.

3.Mishelle Obama

michelle-obama-05f99b947776ef58 SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE

Nampenda mishelle Obama , ni mwanamke mwenye nguvu, mama , mke  na ni kiongozi.  Ni mtu mwenye furaha na mtu wa karibu na watu. Ni mtu wa kuigwa , anaweza kukuongoza  na kupata mwelekeo mpya wa maisha .

4.Sara  Blakel

download SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE

Ni mwanamke ambaye namtamania sana, kutokana na historia yake ya biashara  na bado anaendelea na biashara yake. Anaonyesha kuwa  hata wewe unaweza  kuwa wewe, unaweza kufanya kitu kikubwa. Amua kwamba unataka kujisikia vizuri na  kuonekana vizuri. Na bado utakuwa vizuri kwenye kazi zako.Imani yake ni kuwawezesha wanawake kwenye biashara.

5.Maya Angelou

ABC_Maya_Angelou_ml_131122_16x9_992 SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE

Maya Angelou alikuwa ni mwanamke   mwenye  nguvu ya ukweli na ujasiri,   kwa upendo na huruma , na mwenye kusamehe na mwenye hekima.Inanitia nguvu  kwa hilo, kwa mba hata kwenye mambo magumu ya kiasi gani kwenye mazingira na maisha , bado alikuwa na furaha, mcheshi,  na ni mfano wa kuigwa,  mfano wa kuishi katika katika kutosheka , kufahamu, kufurahia.

Inatufundisha sisi wanawake kuishi kwa kujiamini , kuwa na huruma  panapostahili, tusiwe waathirika, Tusiwe na uchungu mioyoni, au kushindwa au kuchukulia mambo kwa ugumu zaidi kwenye njia zetu, mahali ambapo tunasahau kuwa na ukamilifu wa maisha.

Anatukumbusha kuwa tunaweza kuishi  kwa utoshelevu, kuheshimu uwezo tulio nao, hata tunapokuwa kwenye majaribu . tuweze kuongea ukweli na kuwa na upendo wa kweli.

Alisema ; Mission yake sio kuishi tu, lakini  ni kustawi; na kufanya hivyo ni pamoja na hamu , ya kuwa na huruma , na uchangamfu kiasi  .na mitindo mingine.

6.Lady Gaga

1_66 SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE

Huyu mwanamke kwa kweli , hebu muongelee wewe, maana mimi huenda nina roho  ya tofauti. Ila kusema kweli Ana kitu cha kuigwa.

7.Serena Williams

Serena-Williams-8-1024x614 SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE

Kuna wanawake wengi sana  wa aina hii, lakini mimi navutiwa sana na  Serena Williams, Ana nguvu sana, anauwezo wa kutosha , nampenda , kila kitu anachokifanya kinaonyesha ujasiri wa kike . ni muhamasishaji kwa wanawake

Hawa ni baadhi tu ya wanawake ambao  kwa kweli wananivutia na kunitia moyo , kunihamasisha. Najua hata wewe wapo wanawake ambao wanakuvutia na kukufanya ufuate nyendo zao.Uwe mwenye nguvu na uwezo wa kufanya kila unachoona kinafaa kwa ajili yako na wengine.

482731668 SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUKUHAMASISHA UWE BORA WEWE KAMA WEWE
Women in exercise class, taking break

Toa maoni yako na uwashirikishe na wengine.

Previous WANASAYANSI WANASEMA WATU WENYE AKILI HUWA NA TABIA ZA KAWAIDA
Next HII MILA MOJA INAWEZA KUTUSAIDIA SISI KULEA WATOTO WENYE UTULIVU

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.