Tabia Mpya.


0a053e54-80bd-4617-99c4-31d284e24b1e-455_crime_101_unit_00827r Tabia Mpya.Maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo.

Asilimia 95 ya maisha ya mtu ni tabia yake. Asilimia 5 tu ndio ya ujuzi na maarifa.

Mtazamo wa mtu unajengwa na mkusanyiko wa tabia zake .

Unaweza kutengeneza tabia mpya iliyo nzuri maishani mwako, ili kufunika tabia mbaya zote ulizokuwa nazo.

Kuna Aina 3 Za Tabia,

1.Tabia ya Kurithi.

Tabia zinaweza kurithiwa kutoka kwa wazazi, kama baba  ni mlevi , mtoto naye atakuwa mlevi. Kama anavuta sigara , mtoto atakuwa anavuta sigara, wengi wako hivyo kama baba hajabadili tabia.  Kama mama ana tabia chafu na mtoto wake wa kike atakuwa na tabia chafu vile vile. Ezekiel 16:44  , Neno la Mungu linasema hivi,

Tazama kila mtu atumiae mithali  atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake.

Msidanganyike mazungumzo mabaya huharibu tabia njema , tumieni Akili kama ipasavyo wala msitende dhambi. maana kuna wasiomjua Mungu.

2.Tabia Ya Kutengeneza.

Mitandao ya kijamii ni tabia za kutengeneza,  Kuomba , kuimba, kusifu ni tabia za kutengeneza. Tengeneza tabia ya kusoma neno la Mungu, Tabia ya kujifunza vitu mbalimbali vipya, tabia ya Upendo, Tabia ya kushukuru, Tabia ya kurudi nyumbani mapema, Tabia ya Nidhamu ya mitandao, Tabia ya kumsikiliza mtu na kuuliza maswali baada ya kusikiliza kwa makini, Tabia ya kuamka mapema, Tabia ya kupuuzia mambo kadhaa, sio kuhamaki kwa kila kitu.

Jifunze tabia za Mungu.

Tabia ya Mungu ni Upendo

Tabia ya Mungu ni Kutoa, kutoa ni upendo.

Asili ya Mungu ni Upendo.

3.Tabia ya Mazingira.

Tabia hii ni kuchukua tabia za mitaani, kwa sababu ya kukaa sana kwenye vijiwe, Bar, kwenye  kucheza drafti,  Mfano wa tabia za mazingira ni hizi.

Kupiga mke.

Kuambiwa na marafiki eti usimwamini mke wako

Usimshirikishe mambo yako, Utamwambia nani sasa, kama humwambii mke wako, mwambie mama yako sasa mambo yako, Mama yako ni mke wa baba yako, utamwambiaje mambo yako?

Ndio maana wanaume wa aina hii huwa hawafanikiwi, wanateseka kwa kukosa baraka za mke. Hamsikilizi mke wake, anasema anaongea Pumba. Kumbuka ndani ya Pumba kuna Mchele. Ukikataa pumba ,  Kuna mtu atavumilia pumba na mwisho ataona mchele.

Huwezi kushindana na mwanamke, mwanamke ana akili nyingi kuliko  wewe. Utawezaje kushindana na mtu anayeweza kufanya mambo 10 kwa wakati mmoja?  Kuwa mpole. Halafu maamuzi unafanya wewe.

Anza kujifunza tabia njema kwa kuongea maneno mazuri ndani ya familia yako. Kidogo kidogo utaanza kubadilika. Ndoa haina ladha kwa sababu hutaki kutengeneza tabia mpya. Tengeneza kawaida mpya.

Kama unaona ngumu kusema maneno mazuri kiswahili jifunze haya ya kiingereza ni marahisi kusema kuliko ya kiswahili,

Mwambie mke wako, waambie watoto wako, waambie wazazi wako, marafiki na watu wanaokuzunguka kama hivi.,

I love you

I miss you

Well come

Thank you

Please

Have a nice day

You look nice

I real enjoy

No problem

Excuse me

God bless you, na mengine mengi. najua maneno ya kiswali ulimi unakuwa mzito kuongea maana yana maana nzito. ukiweza sema kiswahili.

Kumbuka kila neno lina sehemu yake. tumia kulingana na sehemu yake.  kama huwezi kujua nitafute tufundishane.

Na kama huwezi kabisa kutamka hata kwa lugha ya kiingereza, Anza kuandika vikaratasi na kumpa muhusika kwa wakati huo.

Huku kote ni kutengeneza tabia mpya.

Tabia inatengenezwa ndani ya muda, Muda ukitumika vizuri utatengeneza kawaida mpya, lakini ukitumika vibaya , utatengeneza tabia mbaya.

Mimi nimetengeneza kawaida mpya, Namshukuru Mungu kila inapofika saa kamili, natumia dakika moja tu kati ya dakika sitini. Natuma maombi yangu kwenye dakika hio moja.

Tengeneza tabia mpya ili uweze kulinda moyo wako kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Mlee mtoto katika  njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

Jinsi gani kijana aisafishe njia yake, kwa kutii na kulifuata neno lako.

Tengeneza kawaida mpya bado hujachelewa.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Unahitaji Msaada Kwenye Mahusiano Yako?
Next Unajihisi Uko Kwenye Umri Gani?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.