UKITAKA MPENYO FIKIRI KAMA MTUMISHI


Easter-Day-15 UKITAKA MPENYO FIKIRI KAMA MTUMISHI

Watu pekee wenye Furaha ya kweli, ni wale tu waliojifunza jinsi ya kufikiri kama mtumishi na kutenda kama mtumishi.

Lakini  Mtumishi wangu Elizabeth, kwa kuwa alikuwa na Roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka Nchi hio aliyoingia; na uzao wake watamiliki.

Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu ajitahidi kuangalia mambo ya wengine, jinsi gani ataweza kufanya kitu kwa ajili ya hao, kuwa na nia ya kitumishi kama  vile nia ya Mungu kwetu.

1.Mabadiliko  ya Akili

Kubadilika kunahitaji sana utayari wa Akili ya mtu.  kufikiri kama mtumishi ni kufikiri kama Mungu anavyofikiri. Mtumishi anafikiri sana kuhusu namna gani atawasaidia watu kuliko anavyojifikiria yeye mwenyewe. Ukiona ndani yako unawaza kupata kwanza kabla hujafanya kitu, tambua kuwa  haupo kwenye kundi la watu  wanaofikiri kama watumishi.  Na kama utaona  nafsini mwako unawaza  kusaidia watu zaidi kuliko kujiona wewe, tayari unafikiri kama Mungu anavyofikiri.

Watu wanaofikiri kitumishi ni wale ambao wanaboresha akili zao kila mara katika kujifunza, kusoma neno, kwenda kwenye semina mbalimbali. wamekua kiakili.  ndio watu  wenye mafanikio makubwa. watu ambao walitambua siri kubwa ya kuwa juu ni kufanya kazi ya Mungu ,kazi ya kumpenda Mungu , Kazi ya kuwapenda watu, kazi ya kupenda mazingira, kazi ya injili.

Kufikiri kama mtumishi, fikiri sawasawa, usiangalie ubaya wa mtu, Tafuta mazuri yalioko ndani yake. Huisha fikra yako kwa kujifunza kutenda mema. Hatimaye ndugu zangu  mambo yoyote yaliyo ya staha , yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwemo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote,  tafakarini haya.

Kama umeumbwa kwa mfano wa Mungu, hutaacha kufanya mapenzi ya Mungu, kwa maana kumpenda Mungu ni  katika kutumikia watu .Kama una upendo hutakosa kazi ya kufanya, kwa sababu Muda unao wa masaa 24 kwa siku.

Angalia sana jinsi unavyoenenda si kama mtu asiyekuwa na akili, bali kama mtu mwenye akili, Ukiukomboa wakati  kwa kwenda kuwasaidia Yatima  na wajane katika dhiki yao  Yakobo 1: 27.   Nenda kwa wagonjwa  wape maneno ya faraja, Nenda kwa Wafungwa waambie maneno ya Mungu na kuwatia moyo, wanakusubiri wewe, Fanya usafi wa mazingira , Mfundishe mtu Upendo wa Mungu .

Hapo sasa ukiwa unafanya hivi vyote utaweza kusema unaweza mambo yote katika yeye akutiaye nguvu. Hapo ndipo utamwendea Mungu kwa ujasiri ili upate rehema na Neema ya kukusaidia wakati wa mahitaji, Hapo ndipo utapata Nguvu ya hoja, kwa kuwa tayari unazo hoja zenye nguvu.  Na hapo ndipo utafikiri kama mtumishi.

2.Mabadiliko Katika Tabia

Ili matendo yako yawe sahihi, katika kufikiri kama mtumishi , ishi ndani ya tabia za Mungu. kwa sababu matendo yote ni matokeo ya  kuwaza kwako, kufikiri kwako,  mtazamo wako, na hisia zako.

Ukiwaza vibaya, utapata picha mbaya, utaongea vibaya, utakuwa na mtazamo mbaya na  utatenda vibaya. Asilimia 100 ya tabia ya mwanadamu ni mtazamo wake.

Tabia za Mungu ni  katika Isaya 11:2. Na roho ya bwana atakaa juu yake , roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza,  roho ya maarifa na kumcha Bwana.  Wagalatia 5:22,23 nayo ni Tunda la roho, Ni  upendo , furaha, amani,uvumilivu ,utu wema, Fadhili, uaminifu, upole na Kiasi.

Tabia hizo ziumbike  ndani ya kila mtu, sio kwa kuongea tu bali katika kutenda.

Kwa hio fikiri kama mtumishi, waza kama mtumishi, tazama kama mtumishi, tenda kama mtumishi kama unataka kubadilika na kufanikiwa katika mambo yako yote.

Kila kutoa kuliko kwema , na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika , wala kivuli cha kugeuka geuka.

Ukimpenda Mungu utafanya kazi zake.

Kama una swali binafsi unaweza kutuma ujumbe tu sio kupiga simu. na kama unapita kwenye changamoto kubwa ambayo huoni mwisho wake , tuma ujumbe  nikusaidie kupitia Neno la Mungu  utapata mpenyo. Neno La Mungu halijawahi kushindwa na halitashindwa . Namba yangu ni hii  0756 662 631

Subscribe ili kupata masomo mapya

Previous MLANGO WA IMANI UMEFUNGULIWA KWA AJILI YAKO
Next MAAGANO AMBAYO MUNGU HUTUMIA KUWABARIKI WATU WAKE

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.