Uko Tayari Kujaribu Kitu Kipya?


AAEAAQAAAAAAAAwkAAAAJDg3MDI5MDYwLTRlMTUtNDY2MS1hMDBmLTY5OTMwYzczYjY1ZA-1024x577 Uko Tayari Kujaribu Kitu Kipya?

Jifunze Kuwa Mtu Wa Shukurani.

Badala ya kulaumu, kulalamika, kusononeka, kujikataa,  jaribu kwenda kinyume na hivyo.  Achana na maombi ya kupigana, kuvunja, kulia, kufunga. zaidi sana anza kuwa mtu wa shukurani.

Watu wanapokuwa wanajisikia kuwa na shukurani kwenye mahusiano yao , furaha yao, kujicommit kwao, hawawezi kukutana na matatizo ya kuachana au kuchukiana.kwa sababu shukurani inakamilifu mambo mazuri na makubwa. inakuonyesha kuwa unatakiwa kufanya vizuri zaidi.

Wanajisikia kukubaliwa na wenza wao na pia ni wazuri . kwa hio kama hujawahi kufanya hivi kabla , mwaka huu 2018  anza kumshukuru mwenza wako  kwa kila jambo ambalo analifanya  kwa ajili yenu. Hauko peke yako . Lakini kama ukijaribu utaona  faida yake ndani ya moyo wako, akili yako na hata afya yako kwa ujumla.

images-2 Uko Tayari Kujaribu Kitu Kipya?

Kuna Hatua mbili rahisi ambazo unaweza kuanza kujaribu kutumia.

1.Andika barua kwa mwenza wako ukijielezea unashukuru kwa ajili ya nini

2.Msomee hio barua

Wakati unaendelea na namba 2, anza kufikiria endapo wewe ndio mwenza wako anakusomea hio barua. Natumaini ungejisikia vizuri sana. Ungependa kusikia barua hio?  Tegemea mwenza wako kujisikia hali hio hio unayoisikia wewe. Lakini kama kwa namna yeyote   ambayo itakufanya ushindwe kusoma barua hio kwa mwenza wako . andika kwa email.

Andika barua hii leo ili kujaribu. Lakini kumbuka hii barua sio ya kuandika kila mara , ila ni kwa ajili ya wale ambao wanaona kuwa kuna  mwanya  ambao umejitokeza , na unataka kuuziba .

Mwambie mwenza wako jinsi gani unamkubali , unakubali kazi zake, juhudi yake ya kazi, upendo alionao kwako na familia,  fikiria kitu ambacho mwenza wako amekufanyia maishani mwako, vitu vizuri, kitu ambacho huwa unakipenda kutoka kwa mwenza wako. vitu vinavyokuvutia .

Ukimaliza kuandika , Subiri wakati akiwa vizuri, wakati ambao hayuko busy , wakati ambao anaweza kusikiliza. Unaweza kuuliza kama unaweza kumsomea barua. mweleze tu kuwa unataka kumfanya ajisikie vizuri na jinsi gani wewe unafurahishwa nae. Hakikisha umeweka kopy kwa ajili yako ili uweze kusoma wakati mwingine  unapohitaji  kujikumbusha kitu.

Watu wengi sana wanaharibu mahusiano yao kwa sababu ya kulalamika bila sababu ya msingi. hawakumbuki kuwa kuna njia hii ya shukurani inayotengeneza mahusiano. Kuanzia leo anza zoezi la shukurani. Sio kwenye mahusiano tu bali katika kila kitu .

Hata kuomba kwako  , anza kubadilisha maombi yako , kuwa mtu wa kumsifu Mungu, kumshukuru Mungu na kumkumbuka Mungu kila wakati. Tena njia nzuri ya kufanya hivyo, ni kila baada ya dakika 60, yaani kila inapofika saa kamili mshukuru Mungu kwa ajili ya mwenza wako, familia, watoto, kazi, wazazi, afya, nyumba, gari na mengine mengi . tumia dakika moja tu. panda mbegu ya muda kwa Mungu kwa kumpa dakika moja kila saa.

Hutakaa ushindwe katika maisha yako kwenye kila  hatua unayopitia.

Utapata KIBALI, ULINZI, AKILI, NGUVU.

Zaidi na zaidi kama utakuwa unaomba Mungu akupe Hekima, maarifa, ufahamu, uwezo wa kuelewa. Pia ukawa na Tunda la roho ndani yako. Upendo, furaha, Amani, Utu wema, Upole, Kiasi  na uvumilivu, fadhili. hutakaa ushindwe na kitu. 

Shukurani, Msamaha, Wema, Upendo na uelewa, ni vitu vikubwa katika mahusiano yako. 

Heri Ya Mwaka Mpya.

Subscribe ili kupata makala mpya.

Previous AKILI YAKO ITAJUAJE KAMA KILA KITU KIPO KWA AJILI YAKO.
Next Kitu Gani Cha Muhimu Sana Katika Maisha Yako Mwaka Huu

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.