Umekuwa Ukipoteza Muda Wako Vibaya?


african_hands_typinge Umekuwa Ukipoteza Muda Wako  Vibaya?

Umejikuta tu uko bussy siku nzima  katika mipangilio yako ya kazi?  Umekuwa ukivuta muda  mara nyingi?

Kama jibu kako ni ndio,  Hutumii muda wako  vizuri.  Inaonekana kwamba umefungwa akili yako  kwenye hio hali uliyonayo sasa. Na kazi hio ndio inakula muda wako na nguvu zako nyingi.

Kwa mfano. Unaamini  kwamba  kucheki emails zako  zinakupa  matokeo mazuri au kukaa kwako kwenye mikutano mingi?  Unaweza kufikiria hivyo.  Lakini mwisho wa siku ni kiasi gani cha kazi yenye faida kwako umekamilisha?

Kwa bahati nzuri , umeona kabisa  kwa kifupi tu kwamba ,  inawezekana kupunguza  vitu visivyo na umuhimu  ambavyo vinajaza nafasi yako  na kukosa kufanya vitu vinavyokuletea mafanikio . Ingawa  kila mtu kabla alipitia huko na kupoteza muda mwingi kwenye kazi za watu wengine.

Unaweza ukawa ni moja ya watu ambao  wanaona kupungua katika  utendaji wao wa kazi  kutokana na kujali sana mambo ya mitandao , Ni kweli lakini usijisikie vibaya. Kila mtu huwa anapotea karibu kila mara kwenye maisha. Na hii ni kwa sababu , kama tutaweza kuwa wakweli ni rahisi kuweza  kufanya vitu vya muhimu  zaidi  kuliko  kufanya mambo yasio na msingi katika maisha yetu.

Ni jumamosi asubuhi na unajisikia kuchoka , Na ndio kwanza  hutaki kwenda kazini kumalizia kazi ambazo ni za muhimu.  Mara unaamua kwenda kupata kahawa nje ya ofisi yako. Ingawa  umeingia kwenye mtego mbaya  ambao haukuwezeshi kufanikisha malengo  yako, umeshindwa kufanya kitu chako kiwe na kipaumbele kwako. Kwa sababu hio , nakuambia kuwa bado unafanya kazi ambayo sio muhimu katika maisha yako.

Kwa mfano ni mara ngapi unafanya kitu chako mwenyewe asubuhi unapoamka kama sio kuchungulia meseji kwenye smart phone yako, kucheki instagram, facebook na vingine. Jibu hapa ni ndio ,  unafanya hivyo kabla ya kazi zako za muhimu. Kwa kesi hio unajikuta unapoteza saa nzima kwa kupitia hivyo vitu visivyo na maana katika maisha yako, unajikuta  hujacheki malengo yako. Wakati mwingine unajikuta vijiweni kuongea umbea wa wanawake au wanaume ,  na hio ndio unaiita mikutano yako.  Ukijakukumbuka muda umepita hujafanya chochote kinachohusu malengo yako.

Sifahamu kuhusu wewe, lakini mimi nimeona baadhi ya watu wanapenda kukusanyika  kwa ajili ya kudiscuss, kuwepo, ili kutatua matatizo  .

Lakini kuna kesi nyingi  ambazo nimeona watu wakipoteza muda kwenye  hio mikutano bila ya sababu za msingi. Unapoteza muda wako na muda wa wengine.

Ingawa kuna mikutano mingine ya muhimu , lakini mingi sio ya muhimu.  ni kupotezeana muda tu.

Kila kitu katika maisha  kina matatizo yake.  na hii inatokana na jinsi unavyofanya kazi zako.

Kama unatumia muda mwingi katika kufanya kazi ambazo sio za muhimu,  Hutaweza kuona matokeo makubwa. Kusema kweli, Uzalishaji wako utakwama. Kwa sababu muda wako umekuwa ukiliwa  kwa kujaribu kufanya  kazi ya mtu mwingine kusubiri ulipwe mshahara.  Sehemu mbaya zaidi ni hii, utajikuta umepoteza muda wako , umri umeenda, hujafanya chochote katika malengo yako.

Utafanyaje kuondokana na hili tatizo?

Tafuta ujasiri wa kuondoka katika mtego huo. Haijalishi  una kazi gani, hutaweza kutumia muda vizuri, masaa yako utatumia kwenye kazi ya mwanaume mwenzako au mwanamke mwenzako. utashuka  thamani kila siku, hutakamilisha lengo lako.

Ukiweza kupata ujasiri tu wa kufanya kitu chako mwenyewe, tayari utakuwa umeokoa muda wako.  Utafanya kitu kilicho sahihi, kitu ambacho tunakiita KAZI sio Kibarua.

Kumbuka kama umekwama mahali huelewi kitu cha kufanya. Unaona kabisa kazi uliyonayo huna furaha nayo, Una malengo hujayafanyia kazi,  Ongea na bosi wako kuhusu kazi yake. Fanya kwa masaa 6 tu na kwa uhakika na kwa juhudi zote. kisha uwe na lengo, fanya kwa mkataba . jiwekee mipango ya  kufanya kazi. Ukifanya kwa uaminifu, muda wa miaka mitatu tu, Utapata  kazi yako mwenyewe.

Ukiona mambo yanazidi kuwa magumu nitafute nikusaidie . tuma  maswali yako, uliza nikusaidie. Zipo njia ambazo zitakusaidia kukutoa mahali ulikokwama. Akili iliyokuweka hapo imechoka. haiwezi kukutoa hapo.

Subscribe kupata makala mpya.

 

Previous Kwa Maneno 3 Tu Unaweza Kumpata Mwanaume Wa Maisha Yako
Next Hii Ni Nzuri Wakati Unapochagua Kujisamehe

1 Comment

  1. Avatar
    skudhany
    February 7, 2018
    Reply

    Nimeipenda hii

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.