Unahitaji Kufahamu Vitu 11 Kuhusu Process Ya Uponyaji


maumivu-ya-hedhi1 Unahitaji Kufahamu Vitu 11 Kuhusu Process Ya Uponyaji

1.Maumivu yapo.

Maumivu hutokea mara, ni kitu kisichozuilika, ni sehemu iliyoumizwa na inahitaji utaratibu wa kupona,  Ili kusonga mbele kutokana na hisia za kuumizwa itabidi utambue  aina ya maumivu. Machozi ya wakati huu sio udhaifu, ni uhakikisho wa nguvu zako; inaonyesha ukweli wake kutokana na maumivu uliyonayo.

2.Hakuna Njia Sahihi Ya kutibu.

Kila mtu hujishughulikia kwa njia yake  tofauti, na wakati tofauti. Maisha sio mashindano ya mbio ya kutaka kujua nani mwenye nguvu  katika kiasi cha muda. Japo process yako ni ya ukimya au  kelele, Ina rangi au haina rangi. Inategemea jinsi maumivu yako yalivyo.

3.Usijitenge.

Ni rahisi kuweza kuwaza mambo mabaya kama utajitenga na watu ambao wanakujali.  Lakini hakikisha unapata muda wa kuwa peke yako wakati mwingine ni vizuri. Kama utaona ni vema kuwa peke yako, toka mwenyewe, nenda sehemu nzuri ya kufurahisha,  nenda dinner, movies.jiunganishe na ulimwengu, hauko peke yako mwenye maumivu.

4.Ongea kuhusu Hilo. Achilia .

Kuongea itakusaidia kupunguza maumivu na kupata ushauri. Au kama unaona hakuna mtu unamwamini, chukua karatasi andika yote yanayokuumiza. ni njia nzuri ya kukufanya uelewe kitu gani kinaendelea kichwani mwako.

5.Jipe Muda.

Muda unaweza usiponye maumivu au vidonda vyote, lakini kila siku kuna kitu kitakuwa kinaungua.Jinsi unavyoishi ndivyo yanavyopotea, ndivyo unavyoshughulikia. Una ujasiri kuliko unavyojijua.

6.Jijali wewe Mwenyewe.

Kuna wakati unaweza kujiona kama umetupwa, umekataliwa, hakuna wa kukujali. Lakini ni muhimu kuujali mwili wako, kuupenda mwili wako kuliko mtu mwingine. Kula vizuri, lala vizuri. meditate, kunywa maji ya kutosha, Usiogope kuomba msaada.

7.Usijione Mkosaji.

Kila mtu hufanya makosa. Mengine ni makubwa kuliko makosa mengine, mengine ni magumu kusamehe na kusahau, lakini hakuna sababu ya kujilaumu na kuona kuwa una makosa, Huwezi kubadilisha kitu ambacho tayari kimefanyika, wewe sio Mungu.  Jifunze kutokana na hayo makosa kwa wakati mwingine. Huko ndiko kukua na kuendelea.

8.Usiogope.

Mara utakapokaa vizuri kwenye hali uliyonayo, hutaweza kuogopa. hapo ndipo utaweza kushinda maumivu. unastahili kujisikia vizuri. hakuna haja ya kuwa na stress katika maisha yako. Utaona urahisi wa kufunika ukurasa na kufungua mpya.

9.Samehe Kila Inapobidi.

Kuna watu ambao utaona ni vigumu kuwasamehe , ambao ndio wamesababisha matatizo maishani mwako, hio ni sawa. ingawa si kila mtu anastahili kusamehewa lakini samehe inapobidi ili uweze kujisikia vizuri, ili uweze kutua mizigo. Upate wepesi wa kusonga mbele.

10.Usijiumize kutokana na Kumbukumbu Zilizopita.

Siku hizi na katika kizazi hiki , ni rahisi kurudisha meseji  ambao zilitokea na hazikuwa nzuri kwako. Fikiria kwamba mapenzi yanaweza kutokea na kuondoka, mapenzi ya uongo siku zote yanaumiza. Hakuna kitu sahihi kinachoonekana sivyo kilivyo. mara nyingi tunajidanganya wenyewe  kwa kuamini tofauti.  Safisha yaliopita, karibisha ukurasa mpya , huhitaji yaliopita zaidi ya kukufundisha kuboresha yaliopo.

11.Unastahili kupata nguvu ya uponyaji, haijalishi ni kitu gani unachotaka kipone. Kila mara , kila mara , kila mara, kumbuka uponyaji una process.

toa maoni yako kusaidia wengine.

kisha Subscribe kupata makala mpya kila mara.

Previous Huwezi Kumbadilisha Mtu Asiyejali
Next Kiini Cha Mbinu Ya Furaha Hakuna Mtu Amewahi Kukufundisha

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.