Unawakumbuka Lakini Huwataki


20228676_803318756497479_8928245539826212951_n Unawakumbuka Lakini Huwataki

Hii ipo kweli, Unaweza kutumia muda wa kutosha kumkumbuka mtu. unatumia  muda mwingi kazini ukiwa unafikiria mikono yao, macho yao, lips zao na sura zao.

Hata usiku umekuwa ukiwakumbuka  na kutamani kama huyo mtu angekuwepo karibu yako wakati huo.

Unamkumbuka .una uhitaji na unataka kumrudisha kwako. Lakini hata humuhitaji. Nafahamu kuwa unafikiri  unamuhitaji, lakini humuhitaji.

Huhitaji hata tabasamu lake , mwili wake hata ucheshi wake.  huhitaji macho yake wala mikono yake, huhitaji moyo wake ili upate furaha. Unajihitaji wewe mwenyewe.

Kuna mamilioni ya watu duniani ambao unaweza kuwapata kama yeye.  wa kweli. na waaminifu. unaweza kumpata aliye bora kuliko huyo. Ipo siku utaweza kumpata mtu ambaye hataweza kufunga mlango wa moyo wake.

Lakini kwa sasa , unaye wewe. na huo ni muujiza wa kipekee, moyo wako bado unafanya kazi, macho yako bado yanaona. mapafu yako yanaingiza hewa. mishipa inafanya kazi bila ya huyo mtu.

Humuhitaji ili uweze kuishi. Na nafahamu kwa sasa ulikuwa unafikiria ni bora kutoishi. unaona bora ufe. Lakini unahitaji kuendelea kuishi, endelea kupigania maisha. Na endelea kustawi.

Unahitaji kujifunza na kuelewa kuwa unaweza kuishi ukiwa mwenyewe.Jifunze kuwa  unaweza kujisikia vizuri zaidi bila ya kuwa na mtu.

Huhitaji macho yao yakuambie jinsi gani ulivyo mzuri na wa kushangaza, tayari ni mzuri. Huhitaji kutiwa moyo, tambua kuwa uko smart na una akili ya kutosha. Huhitaji mioyo yao kusaidia moyo wako ili kujua jinsi gani unapendwa.

Ni kweli kwa sasa unateseka. Sio kitu cha kukataa kirahisi. Sio kitu cha kuzarau. Lakini kumbuka hata hilo litapita tu. Maumivu uliyo nayo yatapita tu. Haina maana kwamba utasahau. Haina maana kwamba utaacha kuwajali na kuwapenda. Ina maana moyo wako utakuwa imara na utajisikia mkamilifu tena. Ukamilifu wako mwenyewe.

Lakini pamoja na hayo, Endelea kutabasamu , kulia na kupumua, kuanguka na kupaa.Endelea kufanya kitu ambacho kinakupa furaha. Endelea kuwa na tunda la uvumilivu.

Ipo siku utafahamu kwa nini.Kwa sababu siku hio, hutawahitaji, wala kuwakumbuka, wala kuwafikiria. Halafu utapata kila ambacho ulitaka kupata. Utapata furaha yako na uhuru wako.

Subscribe kupata makala moto moto.

Previous Madhabahu Binafsi
Next Kwa Nini Unadhifu Wa Mwanaume Humfanya Kuwa Mwenza Mzuri

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.