UNAWEZA KUWA NA NGUVU YA ZIADA YA KUJIZUIA ?


you_can_banner-1024x400-1024x400 UNAWEZA KUWA NA NGUVU YA ZIADA YA KUJIZUIA ?

Unategemea kuwa unaweza kujidhibiti zaidi? Wote tuna wakati ambao tunakosa nguvu ya kujizuia tunapoanguka katika maamuzi yetu. Mbali na kukosa  maamuzi au kuwa na maamuzi mabaya.

Kwa mfano kununu vitu ambavyo havina ulazima , kuhangaika kuweka kipaumbele katika mambo ya kibinadamu yasio na tija. Lakini je unaweza kuboresha nguvu ya kujizuia?

Inapokuja swala la kujizuia watu huanza kufikiria bora kama wangekuwa na nguvu hio zaidi. Nguvu ya kujizuia kufanya jambo baya  inarekebisha na kukuletea ubora wako.

willpower-title-image_tcm7-211639 UNAWEZA KUWA NA NGUVU YA ZIADA YA KUJIZUIA ?

Nguvu hii ni kama misuli, inatakiwa kuifanyia mazoezi kila siku, ili iweze kuimarika tena na tena.

Zoezi hili la kutengeneza nguvu ya kujizuia  itakusaidia kurekebisha  na kudhibiti mambo yako yote.

Kwa hio unatakiwa kufanyia kazi nguvu hii ya kujizuia kila siku.

Wapo watu wanaoamini katika nguvu hii, na mara nyingi wanapogundua kuchoka , hutafuta mbinu zaidi  za kujiimarisha kuliko kukata tamaa.

Haijalishi una nguvu za mwili kiasi gani , kama huna nguvu hii ya kujizuia kufanya mambo yasio na maana katika maisha yako  utajikuta unachoka kihisia .

Ni vizuri kama utajifunza kujidhibiti na jinsi gani utaendelea kufanya hivyo. Kwa hio ni wapi utaanzia inapokuja kuboresha nguvu ya kujizuia?

1.Jitahidi kujidhibiti mara moja moja

Tengeneza zoezi dogo linahusu kujitahidi  kudhibiti. Kwa mfano. Katika  kuboresha  mkao wako, kumaliza kazi, kuacha hasira, kula pasipo na njaa.  fanya kwa zaidi ya wiki mbili au tatu ili kutambua kama kuna mabadiliko

2.Tunza mwili na akili yako

group-fitness UNAWEZA KUWA NA NGUVU YA ZIADA YA KUJIZUIA ?

Inawezekana mwili wako na akili vikawa vimechoka na mfumo  wa nguvu iliopo.  Wakati  hali yako ya kujidhibiti inapokuwa chini ,  tafuta chakula cha kuulisha ili kuutunza angalau kwa kipindi kifupi. Tafuta vyakula vizuri ambavyo vitakupa nguvu na vitamini za kutosha.

3.Fanya Maamuzi Mapema.

Kama ukiwa unapata usingizi mzuri , utaweza kuwa na nguvu ya kujizuia  ya kutosha na utaamka ukiwa full.  Kwa hio ni vizuri kufanya maamuzi asubuhi unapoamka au  kila unapokuwa umepata chakula kizuri . Lakini nguvu hii haifanyi kazi unapokuwa umepata  kinywaji chenye kilevi. Hapa ni baadhi ya watu. kwa kuwa tunatofautiana.

Kumbuka unapotaka kujua  au kuelewa tabia ya mwanadamu ikoje , inafanyaje kazi wakati mwingine, unapojaribu kuonyesha na kuboresha ubinadamu. Ni muhimu kuwa mchunguzi  na kufanikiwa kugundua  kitu gani kinafanya kazi vizuri kwako.

i_can_do_it_scissors UNAWEZA KUWA NA NGUVU YA ZIADA YA KUJIZUIA ?

Utafanya nini ili kuboresha nguvu yako ya kujizuia?

Previous WAKATI MAISHA YANAPOGEUKA UPANDE MWINGINE, MAMBO MABAYA HUTOKEA
Next JINSI YA KUFANYA MAAMUZI YA MUHIMU KATIKA MAISHA

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.