Ushauri Ambao Ningejipa Nilipokuwa Na Umri Wa Miaka 20


tumblr_oealqo7lgJ1qggwnvo1_500 Ushauri Ambao Ningejipa Nilipokuwa Na Umri Wa Miaka 20

Acha Kuwavutia watu.

Nilipokuwa kijana nilifikiri nina kitu cha kuonyesha, nilijaribu kuwavutia watu. Kwa wengine ili waweze kunipenda. Nilihisi nina kitu au njia ya tofauti.

Mfano kama ningekuwa na ucheshi wa kutosha watu wangenifahamu.  Au kama ningeweza kuvutia watu ningeweza kuwa na mvuto. Tatizo lililokuwepo ni kutaka kuthibitishwa   kutoka kwenye chanzo cha muhimu, sisi. tunatafuta kuthibitishwa na wengine. Hii ni mbaya kuliko kitu chochote kama ukiendelea  kuwa na tabia ya kutaka watu wakuthibitishe.

Kuwa Mkweli.

Kuongea ukweli mara nyingi ni kazi ngumu. kuwa na ujasiri wa kujieleza jinsi gani unajisikia  kuhusu mtu mwingine ni biashara ngumu. hii ni changamoto ya  pande zote. kwa mtoto wa kike na kiume. kusema kweli ni ngumu.

Kumbuka yote hio ni mitazamo ya kutokuwa mkweli katika kushirikisha mtu mwingine unachokiwaza. Mtu yeyote akiwa muwazi itampa urahisi mwingine kumfahamu  vizuri bila ya utata  unapoonyesha ukweli wako.

Kama utaongea kutoka moyoni,  bila kujali wengine watafikiria nini , kujiheshimu mwenyewe ni maamuzi mazuri kuliko kujali watu watasema nini kuhusu wewe. utaweza kujifunza hiki kadri unavyokua.

Kuwa Na Ujasiri.

Mara nyingi kama utaogopa kukataliwa hutafanikiwa maishani mwako. Kuwaza kwamba , kama asipokuli,  kama nikijaribu kumshika  na kuamua kunisema vibaya, kama nikifanya hiki na hiki akikataa… itakuaje?

Ni sawa kwa mvulana kuogopa  kukataliwa na mwanamke , lakini isiwe sababu ya kushindwa kujaribu  na kuwa na uhakika na unachokifanya. Fuata shauku ya moyo wako. kama unajisikia kusema kitu sema, unataka kumshika mshike, niamini kinachosema ndani yako ni cha kweli.

Mara zote sikiliza lugha ya mwili wako, hasa macho. nini kinaweza kutokea kama akikusukumia mbali, hakuna tatizo , wala usijisikie vibaya. Furahi kwa kuwa umeonyesha ujasiri. Huko ni kujifunza, wakati mwingine utakuwa  umefahamu nini cha kufanya.

Chukua Muda wako

Kama unataka kuingia kwenye mahusiano jaribu kujifunza kuna nini huko. Nini kinatakiwa kufanyika. soma vitabu vya mahusiano, mfahamu mwanaume au mwanamke kwa kumsoma au kusikiliza maelekezo mbalimbali kwanza kabla hujaamua kufanya kitu chochote maishani mwako.

Kama uko kwenye stage hii ngumu, tumia muda wako kwa kutuliza akili yako , anza kufikiri, kutafuta mawazo mazuri ya kimaendeleo, kila wazo linalokuja akilini mwako Andika chini. Kisha tafutia taarifa za kutosha, maarifa, na ili upate kuelewa vizuri , hakikisha umepata imani ya kitu hicho.

Ukifanya hivyo utajiepusha na kutaka kujaribu aina mbalimbali za wanawake au wanaume kwa kutaka kufanya sex zaidi.

Unataka nini, mahusiano gani unayataka, ni aina gani ya mwanaume au mwanamke unayemtaka?

Jifahamu kwanza wewe.

Hii ni sehemu muhimu sana ya ushauri.  Usipojitambua kuwa wewe ni nani hasa, mahusiano yako yatakuwa ya uongo

Naweza kukuambia hivyo kwa sababu nina uzoefu wa kutosha . kama huna uhakika unataka kitu gani, mahusiano yako hayatadumu.

Mahusiano mazuri yenye afya yanajengwa na  misingi wa uaminifu. chukua muda kutambua ni kitu gani unakitaka maishani mwako. subiri umri usogee mbele . safiri kwanza , jaribu kukaa mwenyewe, hakikisha unajithamini, unajipenda na kujijali.

Vunjwa moyo, jaribu kila mwanamke mwenye sifa unazozitaka wewe, kuwa wazi ili hisia zako zifahamike kama wewe ni mwanaume. kama ni mwanamke hakikisha  hutumii mwili wako vibaya, usijaribiwe jaribiwe kama viatu vya mtumba.

Hakikisha unafahamu ni aina gani ya maisha unayotaka, jitambue wewe ni nani? Unaelekea wapi?  Kuwa na busara, uwe hodari na jasiri, jijengee heshima yako. tengeneza maisha unayoyataka  ili uje ufurahie  baadae.

Kama utaweza kujitambua mapema na kuwa mtu mwenye bidii kujitafuta ajifahamu kwa kujitengenezea maisha mazuri, mtu sahihi atakuja kwako bila ya kuhangaika , wakati ambao umetulia, unapokuwa tayari, na wakati huo utakuwa tayari kukabiliana na changamoto ya aina yoyote na utakuwa umejitengenezea tabia ya maisha  ya ukamilifu.

Subscribe kupata makala mpya

Previous Njia Nzuri Ya Kuponya Huzuni Uliyonayo
Next Nunua Kweli Usiuze,Baki Nayo Ikulinde

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.