VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:


700-524237 © Zoran Milich Toilet Stalls

1.KWA NINI NI VIGUMU KUPUU UKIWA SAFARINI?

Kuna kItu huwa najiuliza mara nyingi nikiwa niko safarini , hata wewe nafikiri ukiwa safarini  ni ngumu kupata  haja kubwa,  kwa nini, kwa sababu ya kubadili mazingira , na kukaa kwa muda mrefu   pamoja na kuvimbiwa  na hewa kujaa tumboni, sababu nyingine ni kula vyakula aina nyingi tofauti tofauti , pamoja na woga wa  njiani kwa kuwa hakuna usalama ukiwa katika hali  hio.UTUMBO huwa unafunga kwa sababu ya kukaa  kwa muda mrefu.

sai-baba-1 VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:

 

2.KUNA WENGINE  WAKIWA MAHALI  WAKICHEKI MUZIKI AU FILAMU HUJIONA KAMA WAPO MAHALI ILIPO.

Ipo hali ya kujisahau wakati wa kuangalia filamu au kusikiliza muziki , ukajiona kama nawe ni mmoja wa kina Diamond na mambo yake ya kila siku, yaani kuna wapo ambao hawapitwi na kitu cha diamond , hufuatilia kama yao, wengine wapo hubeza , wengine wapo hupongeza , mambo ndivyo yalivyo.

ila kama mtu anafanya vizuri apongezwe, asibezwe kama wengine wafanyavyo,  fuata  yaliyo mazuri acha mabaya.

images-10 VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:

3.UPISHI MZURI

Watu wengi hupenda kupika chakula kizuri chenye afya kwa muda maalumu,kupika vizuri ni njia ya kuwa na umakini katika uandaaji wa chakula,  watu wanaojipenda huwa waangalifu sana katika mapishi yao,huandaa chakula chenye kuleta afya kisicho na madhara  yoyote katika mwili wa binadamu.,

kwa mfano vyakula vya mafuta sio vizuri, vyakula vizuri vyenye afya ni vile vinavyopikwa kwa mafuta kidogo na KWA MUDA SAHIHI

download VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:

4.KILA MTU HUWA NA MUDA WAKATI WA SIKUKUU:

Uhuru wa muda ni namba moja katika mitandao tokea asubuhi ya siku ya mapumziko, kwa kuwa wengi huandaa vitu siku kabla ya sikukuu, hufanya manunuzi yote mapema kuepuka msongamano wa watu.

images-11 VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:

5.KAHAWA NI NZURI WAKATI UKIWA UNATAKA MABADILIKO.

Inasemekana kuwa kahawa ni kinywaji kizuri kwa wale watu ambao wanataka kufanya mabadiliko katika miili yao  nkwa kuwa huondoa hamu ya kula chakula mara kwa mara. ina uwezo wa kuondoa hamu ya chakula . kwa hio tumia kahawa kila unapoona unahitaji kula sana. inasaidia hasa wale wanywaji wa pombe kama wanataka kuacha pombe.

6.KUCHANGIA KITANDA NA PAKA

Kuna watu huwa hawajali hata kama paka akienda kulala pamoja nao , wanamwacha tu, na paka huzoea na kuwa kama mahali pake pa kulala,, kwa nini  sasa usimtafutie kitanda chake mwenyewe,  siku hizi kuna magodoro ya paka , mbwa  , unaweza kuwafundisha wawe wanalala sehemu yao  .

inasemekana paka anapopumua  anaweza kukuambukiza magonjwa ya kifua, kwa hio epuka kulala na paka kitanda kimoja.

images-12 VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:

7.ENDORPHINS HAZIKUSAIDII KUWA MWENYE UWEZO WA KUKIMBIA  AU KUWA MWENYE NGUVU NYINGI;

Endorphins ni aina ya dawa ambazo huongeza nguvu hasa kwa wale wanaopenda kukimbia mbio ndefu, lakini sio tu endorphins zikusaidie ,  ukifanya mazoezi ya mara kwa mara utapata nguvu za kuwa na mbio  nndefu , na hatas wale wasio na uwezo wowote ambao hutumia  hizo wanashauriwa kula vizuri na kufanya mazoezi .

images-13 VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:

8.VINUNDU KWENYE MAPAFU NI TATIZO

Wanaume kwa wanawake wote wana vinundu kwenye moyo , ila  wanawake ndio zaidi kuliko wanaume nimesoma kwenye kitabu cha  cancer therapy. kwa hio uchunguzi ni wa muhimu sana kwa KILA mtu .sababu hasa bado kujulikana, inasemekana  sababu mojawapo ni mvilio  katika mishipa ya ndani ,vinaundwa na mishipa ya damu ilioganda pia kuziba kwa ateri za mapafu.( halsa for alla )

exclusiveslungprotein0115ap_732790 VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:

9. WATU ZAIDI YA MILIONI 400 DUNIANI WAMEKOSA UANGALIZI

Watu wengi hawajui kutunza afya zao , kuna makundi ya watu  ambao hawana uwezo na wale wenye uwezo , wale ambao hawana uwezo mara nyingi huwa hawana  pesa ya kujikimu kwa ajili ya kucheki afya zao , lakini hapo hapo hawa ewatu utakuta kwamba wanakula vyakula ambavyo ni vizuri wakati mwingine ila hawajui kuvipangilia,

kwa mfano ukila mchicha na dona lako , ukapata hapo na dagaa , tayari umekula chakula cha maana kuliko aliyekula nyama nono na wali mwingi,  ila kuna wengine hata hio hela ya mchicha na dagaa hana.

ukirudi kwenye kundi la wenye uwezo, wao huona kula mchicha, spinachi au dagaa na maharage ni umaskini , huko ni kukosa maarifa , hapo sasa ndipo  nutajua kuwa unapopata maradhi , utakuwa huli hivyo vitu. utafanya kazi kwa ajili ya watu wengine mwenyewe haufaidiki navyo,

hapohapo kuna wenye akili wenye kujua kutunza afya zao , hula chakula cha kujenga na kulinda mwili. hana tabia ya majivuno eti kwa kuwa ana pesa basi  hawazi kula bamia. ni ujinga . tunza afya yako kwa  kula chakula kizuri .

10.WANAWAKE TUWE MAKINI NA TOILETI PAPER:

Kuna aina nyngi za toileti paper, kuna zingini zina ubora zingine hazina ubora kabisa, tena ambazo hazina ubora hizo ndizo ambazo tunawekewa huko maofisini na makampuni ya usafi , kwa kuwa ni za bei ya chini kwa ajili ya faida zao. wakati huohuo  zinaumiza watu  , hasa wanawake kutokana na  maumbile yetu.

Ushauri wangu ni kwamba tuwe makini na hizo toileti , inasemekana zinasababisha magonjwa kama UTI na hata  kuleta muwasho , mbaya zaidi  zinaweza kusababisha hata cancer, kwa hio tutafute kuwa na akibba kwenye pochi zetu , ukikuta hizo toileti paper za vumbi usitumie, na sio ofisini tu , hata kama umeenda mahali mbali na nyumbani kwako.

images-14 VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:hizi nzuri

download-5 VITU 10 UNAVYOTAKIWA KUVIFAHAMU:     za vumbi hizi.

ongeza na wewe mengine uliyonayo kwa ajili ya kusaidia wengine, toa maoni yako.

 

 

 

 

 

 

 

 

Previous UKIWA MDANGANYIFU NAWE UTADANGANYWA TU:
Next UNAFAHAMU KAMA UNAWEZA KUPONA KIROHO NA KIMWILI?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.