Vitu 6 Hutokea Wakati Mtu Unayempenda Hutaweza Kuishi Naye


images Vitu 6 Hutokea Wakati Mtu Unayempenda Hutaweza Kuishi Naye

Mara nyingi  maana ya Soulmate inatumika vibaya , kwa sababu wengi hufikiri kwa urahisi kwamba ni mtu unayempenda au ni mtu ambaye umeolewa  naye.

Lakini ukweli ni kwamba, na kwa wale ambao wamewahi kukutana au  kupata mtu kama huyo watafahamu hili, ni hisia tofauti kabisa na uzoefu ni tofauti na unapokuwa na mtu unayempenda.

Utagundua dalili mbalimbali unapokutana na huyo mtu, kutakuwepo connection ambayo wote mnakuwa na hisia moja kiakili, kiroho na kiwango cha msisimko. hisia hizi ni ngumu kuzitambua. lakini soulmate wako ana moyo  usiozimika kwako. Mahusiano yanakuwa ni tofauti na sio ya kawaida.

Huyu mtu sio tu atakuwa ni nusu yako , lakini kuna kitu cha ziada anapokupata wewe. kila unapokuwa naye unajisikia umefika nyumbani, hutaweza kuvumilia kukaa bila ya kumgusa mwenzako. Utakuwa unajisikia kama umemfahamu siku nyingi kabla.  Maisha bila ya mtu huyo utaona kama hakuna maisha.  Kitu cha kushangaza hamuwezi kuishi pamoja mara nyingi inatokea hivyo. huenda muda unakuwa bado haujafika. Labda maisha mengine. lakini kwa sasa umejaribu kila mbinu mahusiano yako hayakubali.

Kuagana na mtu ambaye ni soulmate wako ni maumivu yasiopimika, ni kama unaachana naye kwa muda mrefu sana. sehemu hii unajihisi kama kufa anapokuaga.

images-1 Vitu 6 Hutokea Wakati Mtu Unayempenda Hutaweza Kuishi Naye

Hiki ndio kinakuwa kinaendelea pale unapojua kuwa wewe na soulmate wako  hamtaweza kuishi pamoja.

1.Unaweza kupata mtu lakini  hutaweza kuwa na hisia kama zile

Unaweza kupenda  tena  na kuolewa na mtu mwingine lakini  hutakuwa na furaha  wala ukamilifu kwenye maisha yako yote. Kila siku utakuwa unajihisi kupungukiwa na kitu. huwezi kuelezea hicho kitu, lakini kuna nafasi inakuwepo isiyozibika. Halafu haijalishi ni kipindi gani mmepotezana . huwezi kupata upendo kama huo.  hata kama utakubaliana na mimi au hutakubali. huo ndio ukweli.

2.Haijalishi ni miaka mingapi imepita, utakuwa unamkumbuka

Ni ngumu kuondoa kumbukumbu, hasa kama upo kwenye nyakato ngumu maishani mwako. Utakuwa unajaribu kuondoa kichwani mwako lakini ngumu. Akili yako itakuwa ikirudi kila mara  mahali , muda ambao mlikuwa pamoja.  Hata kama ilikuwa ni nyakati mbaya au nzuri mara zote utakuwa umezibeba, hicho ndicho ulichonacho.

3.Utakuwa Mtu Tofauti kabisa

Kuna sehemu inakufa unapoachana na soulmate wako. hutajisikia kama kawaida . utabadilika, hasa kwa jinsi ufanyaji wako wa kazi na wakati ambapo unakutana na mtu mwingine.

Sehemu hii ni ngumu japo utakuwa umepata uzoefu  wa kutosha katika kutambua  uzuri na ubaya wa kuishi na mtu ambaye hakupi furaha kama ya soulmate wako . hata hivyo sehemu hii ina maumivu makali  , utakuwa unakosa kitu kila siku.

4.Kila kitu kinachotokea  utakuwa unaona kibaya.

Utakuwa unajaribu kuweka kila kitu kikae kama ulivyozoea, unataka kifanye kazi . Ni kwa sababu mahusiano sio mazuri, kila mara mtakuwa mnagombana na mwenza wako. utaanza kujiuliza maswali, kama kweli  mwenza wako ana tatizo au wewe ndio una tatizo. kama ukikubaliana na hali halisi  mambo yangekaa vizuri.

5.Kila Mara Anaonekana Kwenye Ndoto Zako.

Miaka na miaka inaweza kupita, lakini soulmate wako atakuwa bado anaonekana  kwenye ndoto zako. Akili yako itakuwa inakukumbusha  na kujikuta unapata maumivu tena.

6.Unaweza kutulia kwenye maisha mapya, lakini soulmate wako utakuwa bado umembeba .

Utasonga mbele, utafurahia maisha, utasafiri, lakini bado atakuwa ni sehemu ya maisha yako. utakuwa umebeba uwepo wao , kumbukumbu zao, vyote utakuwa unabeba kila siku. moyoni mwako na rohoni mwako. Na katika maisha mengine wewe na soulmate wako mtakutana na kuungana tena. lakini sasa jaribun kufurahia maisha , kuwa mkamilifu, penda moyo wako, on ulimwengu, pata mafanikio, uwe mtu mwenye mafanikio makubwa.

Unaweza kukutana na maelfu ya watu lakini hakuna hata mmoja atakayeugusa moyo wako. Lakini ukikutana na mtu mmoja tu ambaye ni soulmate wako , maisha yako yanabadilika.

Previous Hayakuwa Mapenzi Ya Kweli
Next Wekeza Kwenye Ufalme Wa Mungu

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.