Wakati Mzazi Apatapo Mwenza Mpya


Father giving daughter lecture
o-SCOLDING-CHILD-facebook-1024x512 Wakati Mzazi Apatapo Mwenza Mpya
baba anamuonya binti yake

Muda wowote familia  inapokutana na mwingiliano fulani  hubadilika.

kutoka katika hali ya kawaida  kama kifo, talaka, au kuongezeka mtu, kwa mfano kama kuzaliwa mtoto ndani ya familia, au kuna familia zingine baba kuoa mwanamke wa pili, au mama kuolewa  na mume mwingine , wakati huo huo ana watoto tayari .

Hali hii huwa ni ngumu kwa kila mtoto  au ndugu wa familia hio kukubaliana nayo.   Hasa pale anapokuja kutambulishwa kama  girlfriend au boyfriend , ni ngumu  kwa watoto  kiuambiwa huyu ni mama mpya , baba mpya.

Hivi karibuni ndugu mmoja alinielezea jinsi binti yake alivyomwita  girlfriend wake malaya, mwehu, mzinzi, maneno ya ajabu yalimtoka huyo binti tena mbele za watu, hakuweza kuthibiti hio hali,  watu walikuwepo wengi  wamewazunguka, kulikuwa na hisia nyingi  kwa kuwa ni mambo ambayo yalikuwa yanaumiza.

Kwa hio Utafanyaje kama mwanao  amemtamkiwa maneno kama hayo mwenza wako?

Kinapotokea kitu kama hiki kwa sababu ya kupanic unaweza ukamuadhibu vibaya mtoto wako, bila ya kuchukua jukumu la kuongea naye kwanza . Unaweza kuona umefanya vizuri wakati huo lakini je  utakuwa umetengeneza au umeharibu zaidi.

Makwazo hayana budi kuja , lakini angalia usije ukatenda dhambi. usije ukaharibu kabisa. Jaribu kufungua akili yako ili uweze kuelewa vizuri kitu gani kimetokea , hata kama hujapenda  kilichosemwa au kutendwa. Fikiri kwa kina sana utaona kitu gani kimeleta hasira kwa mtoto au watoto.

angry-parent-child-today-tease-150806_113a090aab66bc18f44c0d292fed5bb4-1024x576 Wakati Mzazi Apatapo Mwenza MpyaVaa viatu vyao, vaa kiatu chake , ili uone kinaumiza namna gani au kinampa shida gani huyo mtoto.  Hapo ndipo utakapoelewa jinsi gani alikuwa na hasira mpaka kutamka au kufanya jambo kama lililotokea hapo.

Ni ngumu sana kumkubali mtu mpya kwenye maisha yao kama  walikuwa na mama yao au baba yao , lakini sasa wakiangalia hayupo tena kwa sababu moja au nyingine. watakuwa wanamwangalia mtu mpya kama ni mshindani wao , kama atapunguza mapenzi  yako kwao, kama vile watakosa nafasi kwako.  wanaweza kufikiri kwamba hutaweza kuwahudumia tena, au wataona kama  vile ni badala ya baba yao au mama yao, ni ngumu kukubali kirahisi.

Kama ukjijikuta katika hali hio  au mazingira kama hayo, njia pekee iliyo bora ni kukaa na kuongea nao ili uweze kujua tatizo. Anza kwa kutambua hasira iliyopo. waulize ni kitu gani kinawafanya wawe na hasira , utakapoelewa , waulize  wanajisikiaje kuwepo na mwenza wako mpya.

Wape nafasi ya kuongea ili waondoe woga walionao , baada ya kumaliza kile ambacho kilikuwa kinafanyika kwao. Utaona unaanza kupata majibu ya matumaini.  Au tafuta njia ya kuwafanya wote wakae katika  hali ya kujisikie salama . wahakikishie kwamba hakuna kitakachobadilika, umuhimu wao kwako upo palepale haijalishi kuwa na mwenza mpya. utakuwa karibu yao kila mara  na kuwasikiliza vizuri.

Unapotengeneza nafsi kubwa kwa ajili ya watoto wako, na kujua hisia zao, ni hatua moja kubwa sana  ya kumtengenezea mwenza wako mpya nafasi yake ya kukubalika kwenye familia yako  maisha yako yote. Mara tumaini hili likiwepo watoto wataanza kumkubali mwenza wako na kujiona kama hawakupotelewa na mtu bali wapo kawaida.

Natumaini kwa wale wenye  mazingira haya magumu wameelewa vya kutosha. Nikupe tu angalizo . Bila Mungu Hutaweza kufanikisha haya yote . Kila jambo lako mshirikishe Mungu  akufanyie wepesi .

Subscribe.

Previous Mistari 27 Ya Neno La Mungu, Kila Mwanamke Anayehitaji Upendo, Uhakika Na Nguvu
Next Mambo Ya Kukumbuka Wakati Unapohisi Kuumizwa Na Upweke

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.