Wakati Unapofika Wa Kubaki Mwenyewe, Ni Kwa Ajili Ya Kujiboresha


woman-living-alone-16x9-1024x576-1024x576 Wakati Unapofika Wa Kubaki  Mwenyewe, Ni Kwa Ajili Ya KujiboreshaUtafika wakati unajikuta mwenyewe nyumbani,  Usiku uko mwenyewe unapojifunika blanketi na kuweka akilini mwako kuwa uko alone.

Unapoanza kuhisi kuhitaji mtu wa kukukumbatia, kukushika,  unahitaji kujifunza  kujikumbatia mwenyewe kwa mikono yako,  Kupendana kupo, lakini hakuna mtu wa kukusaidia  kujielewa wewe kama wewe, Hakuna.

Unahitaji kuwa mwenyewe unapokuwa umekosa furaha, unapopitia madhaifu mbalimbali, unapokuwa unafikiri ipo siku mtu atajitokeza anayekupenda jinsi utakavyo.  lakini ni vizuri kama utajishughulikia  hali hio ikaisha. kwa kuwa hakuna mtu ambaye ataweza kukuomnyesha upendo wa kweli zaidi ya wewe kuanza kujipenda.

Tengeneza tabia ya kujitambua , kujitafuta,  kujipata  na kujiokoa nafsi yako kwa kutumia juhudi ya Mungu.

Unahitaji kuwa mwenyewe wakati mwingi, sio na rafiki, ndugu,  mume au mke. wala kitu cha kukufanya ujisikie vizuri.

Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa anahitaji kupata mtu anayempenda. Yaani anatafuta kupendwa.! nilibaki namshangaa moyoni mwangu, halafu  ukimwangalia utadhani ni mtu anayejifahamu kumbe hakuna kitu.  Akasema  anataka mtu ambaye atamkumbatia ajisikie vizuri.  Ngoja nikuambie siri.  Kuna kanuni nzuri inasema hivi.  Kitu ambacho unataka ufanyiwe na watu, anza kuwafanyia wao kwanza, ndipo utapata unayotaka kupata.  Apandacho mtu ndicho atakachovuna.

Soma Neno La Mungu. Mathayo  7:12. pamoja na Wagalatia 6:7.

Unahitaji kuwa mwenyewe kwanza bila kuangalia wanadamu kukusaidia . japo kuna maumivu makubwa , lakini  tambua ya kuwa ni wakati wa kujifunza, kumjua Mungu, Kujitambua.  kupata mafunuo, kusikiliza sauti ya Mungu.  Kila kitu kipya huwa kina maumivu , Hakuna mafanikio yanayokuja kwa urahisi. chochote unachotaka kuanza , kilicho kizuri, kinahitaji uvumilivu. uvumilivu ni Tunda la Roho.

Muda mwingi utakaokaa mwenyewe ,  utajifunza kuishi wakati uliopo, na wakati ujao tu. hutakuwa mtu wa kukumbuka yaliopita bali  yajayo ambayo  ndio maisha pekee ya imani ya mtu  kufanyika. Imani ni kufanya kitu sasa kwa ajili ya kesho.

Hata siku moja usijitaabishe kwa ajili ya kutaka mtu fulani akupende maishani mwako.  wewe ndio mtu pekee wa kujifanyia mambo mazuri kwanza.  Kanuni inasema Mpende jirani yako kama nafsi yako. Ina maana kwamba kama huipendi nafsi yako sio rahisi kumpenda mtu mwingine.

Anza na wewe mwenyewe. kujitaabisha kwa ajili yako.  usiwe mtu wa kutaka kuonewa huruma . Acha kabisa. . Ngoja nikuambie kitu. Hekima ya Mungu iko hivi,  Unaposikiliza neno na kulifanyia kazi , utafananishwa na mtu  mwenye Akili. aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba, mvua zikaja, pepo zikavuma, lakini nyumba ile haikuanguka kwa kuwa ilijengwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye neno  na asilifanyie kazi  atafanana na Mpumbavu, ambaye alijenga nyumba yake juu ya mchanga, mvua ikaja, upepo ukaja na kuiangusha  nyumba ile, na anguko lake likawa kubwa .

Akili yako itakuwa safi kama utajitahidi  kujiweka sawa mwenyewe, kwa kujifunza neno la Mungu ,  Neno linasafisha akili. Ndiposa utaiona Hekima ya Mungu ndani yako. Hekima ambayo itakupa Ufahamu  wa kutosha katika maisha yako. Hekima haikai kwa mtu mjinga.  Kwa sababu mtu mjinga mambo yanapobadilika   huchanganyikiwa asielewe la kufanya. kwa kuwa hakujifunza  kujidhibiti mwenyewe.

Ndio maana ni muhimu kuishi kwanza mwenyewe kabla hujaanza kukaribisha watu wengine kwenye maisha yako.

Unahitaji muda wa kujifunza kuvaa viatu vya wengine  wanapokuwa wanapita kwenye changamoto.  Unahitaji muda wa kujitambua wewe ni nani, unataka kuwa mtu wa aina gani.

Jifunze kuwaamini watu,  kujali moyo wako kuliko kitu chochote.  usimpe mtu moyo wako. Mpe Mungu tu.  unahitaji utulivu, kujua sasa ni wakati sahihi, na huu sio wakati sahihi kufanya jambo fulani.

Wakati unapokuwa mkamilifu, unapokuwa na mapungufu, madhaifu, unapovunjika moyo. hivi vyote unatakiwa kuvifahamu jinsi gani ya kukabiliana navyo kabla ya kukaribisha mtu mwingine maishani mwako.

Hapo ndipo utagundua kuwa , kujifunza  maisha ya single ni vizuri, utapata ufahamu mkubwa.

 

Previous Mambo Ya Kukumbuka Wakati Unapohisi Kuumizwa Na Upweke
Next Kukumbatiana Inaweza Ikawa Ni Njia Nzuri Ya Kumaliza Tatizo

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.