Wanawake Wanatakiwa Kusaidia Wanawake Wengine


cae2edcc3d413adeeb021862d2cf1615-empowering-women-quotes-supportive-women-quotes Wanawake Wanatakiwa Kusaidia Wanawake Wengine

Kwa uhakika upi wanawake wanaweza kushiriki kitu kwa pamoja  bila ya kuwa na wivu na mwenzake? kwa hali kama ya ufahari, utajiri . Haishangazi kuona wanawake wengi wapo kwenye urafiki wa kuonyana.

Tunaonyesha kuwa na urafiki  kwenye umma lakini ndani kila mtu amebeba siri kubwa ya wivu. tunakuwa na hali ya kuchanganyikiwa  kwa kuona mafaniko ya mwingine . Hatujui kutoa pongezi ya kutoka moyoni , ya kweli.

Tunapenda kulalamika kuhusu maisha yetu ya kila siku na kutazama vibaya waliofanikiwa na kuwasema vibaya badala ya kutambua kwamba   utatuzi  unaanzia katika ushirikiano mzuri na jitihada za  kujitambua wenyewe.

Tunachangia matatizo wenyewe kwa kutaka kushindana  bila kujua kuwa kila mtu ana njia zake za kufanikiwa katika maisha yake. Ni vizuri kama ukahitaji kushirikiana na mtu mwenye uwezo zaidi yako ili uwezae kufahamu japo kidogo ni njia ipi unaweza kupita ili ufanikiwe.

Kila mara tunachangia matatizo hasa pale inapotokea kumsaidia mwanamke mwingine kwa kujionyesha nani zaidi.  kujilinganisha bila sababu.  lakini tunachagua kutofanya chochote katika hilo.  Bora isiwepo nafasi ya  mwanamke ambaye hataki kumsaidia mwanamke mwenzake.

Huenda mwanamke mwenzio kapata cheo kazini , ni pongezi kwake.  bora kama utahitaji kujua ni njia zipi ametumia kufikia hapo alipo sasa. Na wewe ujitahidi zaidi  na uamini ipo siku utavuka sehemu na kufika unakotaka kufika.

Business-women-with-blank-sign-1-1024x584 Wanawake Wanatakiwa Kusaidia Wanawake Wengine
wanawake wafanyabiashara

Huenda ni rafiki yako amefanikiwa kupata mchumba na wewe hata mtu wa kutoka naye mara moja huna.  Ni bahati yake , Mfurahie, mpongeze kutoka moyoni mwako. kwa sababu ukiweka kinyongo  utaendelea kukosa kila siku. Msaidie katika maandalizi yake  ya kuolewa, mtie moyo badala ya kumkatisha tamaa.  Siku ya harusi yake hutajilaumu, utafurahia pamoja naye kwa kuwa ulikuwa karibu naye kwa kila pito lake.

Huenda ni kitu kingine kikubwa, labda unakabiliana na afya ya mwili wako na unaonekana kulemewa.  Huenda familia yako imekutana na mambo ambayo hayawezekani na ungependa  kutatua hilo. Kumbuka kuwa hakuna kisichowezekana kwa Mungu. Huenda umepata mimba bila ya kutarajia, umefanya mapenzi na ikatokea. unaogopa kujionyesha kwa watu.

Ni rahisi kutazama kila sehemu na kujiona ni wewe tu unateseka . Kila mtu anaonekana yuko vizuri ila ni wewe tu umezidiwa na matatizo, Hata wao sio wakamilifu.  huwezi kujua ni matatizo gani wanapitia kwa siri.   Pia huwezi kujua wamepitia kitu gani kufikia mahali walipo.  hujui wataishia wapi baadae.

Rafiki yako ni mtu wa karibu na ni vizuri kusherehekea pamoja .kusiwepo mashindano kati yenu. mwanamke  huyo atakusaidia .ataweza kusimama upande wako siku moja. Atakuinua wakati unapoanguka, atakusaidia kufikia ndoto yako. atakupenda wakati wa raha na wakati wa shida.  Tamani kuwa na rafiki kama huyu mwenye kukuonyesha upendo na kukusikiliza .

Onyesha  huruma na umuhimu. Weka simu yako chini unapomsikiliza  na msome ufahamu shida yake.   Nenda ndani zaidi kama utahisi kuna tatizo. Vaa uhusika  kama unaweza. Wengi wa wanawake huficha maumivu na kuonyesha tabasamu la uongo. kama utaweza kutambua hilo  ni vizuri kumsaidia. Wote tuna mizigo  tunayopita nayo katika maisha haya. lakini tunazidiana jinsi tunavyoweza kukabiliana nayo. Hakuna mtu anayepita kwa urahisi. carefree life. Huenda mahangaiko yako yakawa tofauti na wengine wanaokuzunguka, lakini sote tunapita katika hayo.

Haitakuwa kitu kizuri kama tutaweza kusaidiana kila mmoja kubebeana mizigo badala ya kuwa na Wivu?

Share  kwa wengine.

 

Previous Mambo Madogo 10 Ni Muhimu Kukumbuka Ukiwa Katika Safari Ya Maisha Yako.
Next Msichana Mwenye Ujasiri Anafahamu Kwamba Maisha Yanasonga

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.