Wekeza Kwenye Ufalme Wa Mungu


Kingdom-of-God Wekeza Kwenye Ufalme Wa Mungu

Tunafundisha kumpenda Mungu, Kumpenda jirani na kuipenda nafsi yako,  Tunafundisha vitu ambavyo binadamu ameruka, amesahau, hakufundishwa kabisa. nini cha kuwekeza kwenye ufalme wa Mungu…

Bali utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake. Na mengine yote mtazidishiwa. Mathayo 6.33

Kitu gani cha kuwekeza kwenye Ufalme wa Mungu…

1.Muda -Time.

Unaweza kukosa imani, upendo, furaha ukatafuta  na kuvirejesha endapo utakuwa na muda. Lakini ukipoteza muda hutaweza kurudisha. Tumia Muda wako vizuri katika kufanya kazi za Yesu na kazi za Adamu.

Kazi za Yesu ni kuondoa watu kwenye dhambi. kazi za Adamu ni kutunza mazingira.

2.Imani Yako.

Weka imani yako kwenye Ufalme wa Mungu. Nguvu ya imani yako ipo ndani yako, itambue imani ilioko ndani yako. Maisha yako yanategemea imani yako. Usiogope kuhusu watu watasema nini kuhusu wewe unapowekeza imani yako kwenye Ufalme wa Mungu.Kuwa na uhakika na unachokifanya.

Uwe na imani kila mahali palipoandikwa amini neno la Mungu , ina maana uamini kazi za Mungu. Mungu yupo nawe kila mahali. hayupo kanisani, msikitini wala milimani. anakula nawe, anatembea nawe, anaongea nawe, Amini tu.

Matt-633-1024x490 Wekeza Kwenye Ufalme Wa Mungu

Usilazimishwe kuamini kitu usichokiamini. Wekeza imani yako kwa Mungu. Humtumikii Mungu anayekuja na kuondoka. Unamtumikia Mungu aliye Hai. Amini yuko nawe.

Iko nguvu katika kuamini. Haijalishi una imani gani ndani yako. mithali 23:7

3.Upendo

Wekeza Upendo kwenye ufalme wa Mungu.

Mpende Mungu, mpende jirani yako kama nafsi yako. ipende nafsi yako. mathayo 22:37.Upendo ni kitu kigumu. tunda gumu ni upendo. Tazama ni watu gani wamekuzunguka. Kuna  tatizo ndani yako Tubu, Samehe na ujisamehe mwenyewe. Mathayo 6:24.

4.Ujasiri.

Ujasiri ni bima ya maisha yako. Usiwe mtu wa kufikiri watu watasema nini juu ya kuwekeza kwenye ufalme wa Mungu. Kuwa jasiri. fanya kazi za Mungu kwa ujasiri. Kazi za Mungu zinalipa kuliko kazi zingine. wekeza kwenye ufalme wa Mungu ujasiri wako.

 

Previous Vitu 6 Hutokea Wakati Mtu Unayempenda Hutaweza Kuishi Naye
Next Utajuaje Kama Mwenza Wako Hakupendi

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.