YESU NA PASAKA: KWA NINI KUFUFUKA NI UKWELI MUHIMU ULIMWENGU?


2017-easter-images YESU NA PASAKA: KWA NINI  KUFUFUKA NI  UKWELI MUHIMU ULIMWENGU?

Siku ya leo ni muhimu kwa Wakristo wote Ulimwenguni  ,  kusherehekea kufufuka kwa  Yesu Kristo, na hili liko wazi.

Kufufuka tu kunaleta maana  ya kwanza ya kuelewa  kwamba ni kitu gani kilichohubiria hapo mwanzo. Hili ni tukio la furaha , Wakristo walichukua  hii siku kuwa ni ya furaha  na ni muhimu sana katika maisha yao.

Ni ipi injili ya Wakristo?  Ni habari nzuri ,katika historia ya ulimwenguni, Mungu Yupo pamoja na sisi kwa jina la Yesu ,ambae tunaweza kumfahamu, kumpenda,  na kumtumikia

Kwa kupitia yeye tumetakaswa na kuponywa , na kupewa ufahamu mpya . tumeondolewa katika mizigo mikubwa ya  hofu, woga, kutojiamini, na kukata tamaa.  Amefanyika njia ya  ukweli na uzima.

Injili ya Yesu ni ya kweli , unaweza kuamini au usiamini hivyo. Lakini kama mkristo ,  tunaamini  kwamba  sio tu  ukweli; ni kitu muhimu na cha kweli Ulimwengu mzima.

Hiki ndicho ambacho tunatakiwa kukionyesha   kwa vitendo na kwa maneno yetu kuwa tumepona na  kufanywa upya ndani ya Yesu.

giphy-1 YESU NA PASAKA: KWA NINI  KUFUFUKA NI  UKWELI MUHIMU ULIMWENGU?

Ni kitu cha kufahamika Ulimwenguni sio kwenye mipaka ya  Makanisa yetu tu. Sio kitu cha kufichwa.

Na ukweli  alipofufuka tu kutoka kwenye kaburi  alijionyesha kwa wanafunzi wake  na kuacha  ukweli  wenye nguvu  kwao kuhusu kufufuka kwake.

1.Ufufuo ulimdhihirisha Yesu kuwa ndiye mwenye mamlaka Ulimwenguni.

Yesu alipojionyesha tu kwa wanafunzi wake , neno la kwanza alilosema kutoka  kinywani mwake lilikuwa , ‘’Nimepewa mamlaka yote Mbinguni na Duniani. Ufufuo ulikuwa ni uhakika wa maandiko.

Kwa hio Kuonekana kwake ilikuwa ni muhimu kutokana na  uhitaji wa kutaka kufahamu  mabadiliko  ya Ulimwengu.

Wengine wanafikiri kuwa mamlaka ya mwisho yanatoka   serikalini

Wengine  yanatoka kwenye soko huru.

Wengine wanafikiri mamlaka ya mwisho yanatoka  kwenye hali ya ndani.

Lakini hakuna mamlaka  yenye nguvu , Yesu ndio mwenye mamlaka yote, kwa sababu kila mtu husema kuwa  anatafuta mwanga wa njia . Mwanga wa njia ni nani kama sio Yesu.

Ana mamlaka kuliko kitu chochote.

2.Kufufuka kwake  ina kamilisha kila mtu .

Kitu cha pili ambacho Yesu alikisema kwa wanafunzi wake  ni kwamba , wanatakiwa kuuambia Ulimwengu wote kuhusu  kufufuka kwake na  kuwafundisha  kushika maagizo yake.

Kama ndio kweli kuwa  Yesu ndio mamlaka ya mwisho . Ameondoa nguvu zote za giza . ni jukumu letu kufahamu hilo.

3.Kufufuka kwake inatukumbusha sisi kuwa  tumefufuka kutoka kwenye taabu, magonjwa, mawazo mabaya, kukata tamaa na magomvi.

Amesema atakuwa pamoja nasi kila mahali . kazi yetu ni kuamini tu.

Kitu kizito na kizuri ‘’Kimetokea Ulimwenguni’’ Kitu ambacho tunakifanya siku ya leo pamoja na watu wote  kusherehekea  pamoja nasi  katika kuadhimisha  kufufuka kwa Yesu Kristo.

Nawatakia Siku Kuu  njema ya Pasaka.

Previous MSAHAMA NI KWA AJILI YAKO KWANZA
Next SABABU AMBAYO INAKUFANYA UVUTIWE NA MTU SIO TYPE YAKO

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.